KESI INAYOMKABI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA YAKWAMA KUENDELEA KUSIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA YA CHOMA Inbox x

  Masama Blog      

Na Jumbe Ismailly IGUNGA

KESI inayomkabili Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Peter Onesmo Maloda ya kuingia kwa jinai kwa kuvamia shamba la Tungu Ntegwa imeshindwa kuendelea kusikilizwa katika Mahakama ya mwanzo ya Choma kutokana na Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Ziba, Goodluck Pallangyo kutofika kwa ajili ya shughuli hiyo.

Hakimu Pallangyo amepangiwa kusikiliza kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya mwanzo ya Kata ya Choma na kusajiliwa kwa namba 65/2019 baada ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Choma,Simon Dominick Malima aliyeanza kuisikiliza awali kujitoa kwa hofu ya kutotenda haki kwa kuwa mmoja wa washitakiwa hao ni jirani yake.

Katika maelezo ya shitaka lao inadaiwa kwamba dis,16,mwaka jana saa tatu asubuhi katika maeneo ya Kata ya Choma, washitakiwa kwa pamoja,Peter Onesmo Maloda na Ndekwa Mina Usukani walikutwa wakilima shamba la mlalamikaji Tungu Ntegwa mkazi wa Kijiji cha Choma bila idhini yake,huku wakijua kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Hata hivyo washitakiwa hao baada ya kusomewa shitaka lao walikana na kwamba washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana ya shilingi 500,000/=(laki tano) kila mmoja na mdhamini mmoja.

Akiahirisha kesi hiyo ambayo ilikuwa ianze kusikilizwa kwa mara ya kwanza,Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Choma,Malima alisema kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Igunga,ameihamishia kesi hiyo katika Mahakama ya Kata ya Ziba na kwamba itaendelea kusikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo.

Baada ya Mahakama kutoa maamuzi hayo ndipo mlalamikaji katika shauri hilo alisema kuwa hana uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 50 kwenda na kurudi ilipo mahakama hiyo kwa kuwa hana uwezo wa kifedha na hana usafiri ikilinganishwa na mtuhumiwa namba moja ambaye yeye hutumia usafiri wa gari la Halmashauri ya wilaya hiyo,hivyo anaiomba Mahakama ya wilaya kuirudisha kesi hiyo Mahakama ya kata ya Choma.

Aidha Ntegwa aliiomba pia Mahakama hiyo itoe amri ya kusitishwa matumizi ya shamba hilo hadi hapo kesi hiyo itakapomalizika kusikilizwa na kutolewa maamuzi.

Akitoa maamuzi ya maombi hayo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo,Hakimu huyo alimushauri mlalamikaji kupeleka maombi yake kwa maandishi kwa Hakimu wa wilaya ya Igunga kuhusu kesi hiyo kurudishwa tena katika Mahakama ya mwanzo Choma na kuhusu amri ya kusitisha matumizi ya shamba hakimu huyo alimtaka mlalamikaji huyo kupeleka ombi hilo kwa Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Ziba kwa maamuzi zaidi.

Kwa upande wake mshitakiwa namba moja,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Peter Onesmo Maloda aliiomba Mahakama hiyo kubadili tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo imepangwa kuwa Jan,10,mwaka huu kutokana na siku hiyo kuwa atahitajika kuongoza kikao cha kamati ya Mipango,Fedha na Uchumi ya Halmashauri ya wilaya ya Igunga.

Hakimu Malima hata hivyo alimshauri mtuhumiwa huyo kumtuma mdhamini wake siku ya kesi ili aweze kwenda kutoa taarifa Mahakamani hapo.dhamana za washitakiwa hao zinaendelea hadi jan,10,kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika Mahakama ya mwanzo ya Kata ya Ziba.


Ni Jengo la Mahakama ya mwanzo ya Kata ya Choma,wilayani Igunga,Mkoani Tabora kulikofunguliwa kesi ya jinai namba 65/2019 dhidi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,PETER ONESMO MALODA akikabiliwa na tuhuma za kuvamia shamba la Mkazi wa Kijiji cha Choma
Ni baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Choma,wilayani Igunga waliohudhuria kusikiliza kesi ya diwani wao wa Kata anayekabiliwa na tuhuma za kuvamia shamba
Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga ambaye pia ni diwani wa Kata ya Choma,Bwana Peter Onesmo Maloda akibuni mbinu ya kukwepana na waandishi wa Habari ili asipigwe picha baada ya kesi yake kuahirishwa katika Mahakama hiyo (Picha zote Na Jumbe Ismailly)


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39R7bnl
via
logoblog

Thanks for reading KESI INAYOMKABI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA YAKWAMA KUENDELEA KUSIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA YA CHOMA Inbox x

Previous
« Prev Post