KERO ZA WANUNUZI ZATAJWA KUONGEZA CHANGAMOTO KWENYE ZAO LA TUMBAKU

  Masama Blog      

WANUNUZI wa zao la Tumbaku wametajwa kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya zao hilo kutokana na kero ambazo wamekua wakizitoa wakati wakifanya manunuzi na hivyo kuongeza changamoto kwenye biashara hiyo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku, Stanley Mnozya wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Mnozya amesema kero hizo zinasababishwa na kesi baina ya wanunuzi wa tumbaku na  Tume ya ushindani.

Amesema makampuni matatu kwa pamoja yanadaiwa kiasi cha shilingi Trilioni Saba kiasi ambacho kinatokana na tume ya ushindani kubaini kuwa kampuni hizo hazikuonesha ushindani katika biashara ambapo kiasi hicho kimekuwa kikubwa sana .

Aidha Mnozya   amesema kuchelewesha urejeshwaji wa kodi ya ongezeko la thamani  VAT ambapo kampuni hizo zinaidai serikali tangu mwaka 2016 takribani 42.4 bilioni.

Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kulifanyia kazi suala hii na hasa ahadi ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli wakati akizungumza na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali kuwa marejesho hayo yatafanyika baada ya uhakiki.

Hata hivyo Mnozya ameiomba serikali  kutatua changamoto hizo kwa wakati ili kuziondoa  ambazo zimekuwa zikiikabili na kuithiri sekta ya tumbaku kwa kipindi kirefu sasa.

Amesema kama hatua za utatuzi hazitachukuliwa kuna hatari ya wanunuzi kushindwa kuendesha biashara ya tumbaku kulingana na kiasi cha madeni wanachotakiwa kulipa kuwa kikubwa.
Pia zitarudisha nyuma jitihada za bodi za kutaka kuongeza kilimo cha tumbaku kufikia tani 150,000 ifikapo 2024/2025.

Mnozya amemuomba Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga  kukutana na Waziri wa Viwanda na Biashara ili kujadiliana namna ya kupata masoko ya nchi za COMESA zikihusisha  Misri, Algeria na Sudani kutokana na uhitaji mkubwa wa tumbaku katika nchi hizo.

“Nchi za COMESA wanahitaji tumbaku ya Tanzania lakini  hatuna uanachama na nchi hizo” alisema Mnozya.

Awali amebainisha kwamba kufikia Desemba 15/2019 tani 70,087 zenye thamani ya fedha za kitanzania 230,367,663,073 zimenunuliwa na kuvuka lengo la kununua tani 55,000 huku ajira ikiongezaka na kufikia 1,400,000.
 Wadau mbalimbali wa kilimo wakifuatilia mkutano wa pamoja wa kujadili zao la Tumbaku uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkurungezi Mkuu wa Bodi  ya Tumbaku Stanley Mnozya akizungumza katika moja ya vikao vya kutetea maslahi ya Tumbaku vilivyofanyika jijini Dodoma.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3aNpQB2
via
logoblog

Thanks for reading KERO ZA WANUNUZI ZATAJWA KUONGEZA CHANGAMOTO KWENYE ZAO LA TUMBAKU

Previous
« Prev Post