KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY KUANZA LEO ZIARA YA KIKAZI MKOANI KIGOMA

  Masama Blog      
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kuanzia leo Januari 17 - 19, 2020.

Leo Januari 17 ,2020, Katibu Mkuu anatarajiwa kuwasili Uwanja wa ndege Kigoma Mjini kuelekea moja kwa moja wilayani Uvinza kata ya Kazuramimba ambapo atazungumza na wajumbe wote wa mkutano Mkuu wilaya ya Uvinza, Wazee, mabalozi, viongozi wa kata na matawi pamoja na mabaraza ya jumuiya zote wilayani hapo.

Aidha hapo kesho Januari 18,2020 Katibu Mkuu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu maalum wa kupokea taarifa ya kazi za Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini wilayani Kigoma.

Atamalizia kwa kikao cha mabalozi wote wilaya ya Kigoma kesho kutwa tarehe 19 Januari, ambapo Katibu Mkuu atagawa vitambulisho kwa mabalozi wa wilaya hiyo ikiwa ni mfano kwa mabalozi wote nchini.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NvzCh2
via
logoblog

Thanks for reading KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY KUANZA LEO ZIARA YA KIKAZI MKOANI KIGOMA

Previous
« Prev Post