Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Yatembelea Kiwanda cha ALAF.

  Masama Blog      

Wajumbne wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma, wakiangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam walipotembelea ijumaa
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Kiwanda cha ALAF, Wilberforce Msokwa akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bune ya Kudumu ya Mitaji ya Umma walipotembelea kiwanda hicho.
Meneja wa Usalama pakazi wa Kiwanda cha ALAF, Fredrick Nowi (katikati) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kuduma, Dk Raphael Chegeni (kushoto) wakati wajumbne wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hichoFundi Mitambo na Uzalishaji wa Kiwanda cha ALAF, Paul Luambano (kulia) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma jinsi mitambo inavyofanya kazi wakati kamati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwandani hapo kuangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika

 
 
==========  ========  =========
 
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Raphael Chegeni, leo imefanya ziara katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es salaam. 

Madhumuni ya ziara hii ni kuipa Kamati hiyo uelewa zaidi kuhusu shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zinazofanywa na kiwanda hicho.

Tarehe 14 Januari mwaka huu, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Dipti Mohanty alipata mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo ya Bunge ya Uwekezaji, ambapo alipata fursa ya kuelezea mafanikio ya kampuni hiyo na changamoto mbalimbali za kibiashara.

Kamati hiyo iliipongeza ALAF kwa mafanikio makubwa iliyopata hivi karibuni, na kuahidi kuitembelea kampuni hiyo, ahadi ambayo imetimizwa leo na Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe wote.

Katika ziara ya leo, Kamati imepata fursa ya kutembelea kiwanda cha ALAF na kujionea hatua za uzalishaji, bidhaa na huduma mbalimbali. Pamoja na kukutana na baadhi ya wafanyakazi wa ALAF, pia walitembelea kituo cha afya kinachotoa huduma za matibabu kwa wafanyakazi na familia zao,.

Mtendaji Mkuu, Dipti Mohanty ameishukuru Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kwa kupata muda wa kutembelea ALAF. Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kujenga Tanzania ya viwanda, na kuikaribisha Kamati hiyo kutembelea ALAF tena.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe. Raphael Chegeni, alisema wamekuja kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia ukuwaji wa sekta ya viwanda pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa nishati ya umeme wa hakika pamoja na malipo ya VAT zinazodaiwa kutoka kwa mamalaka ya mapato TRA.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RSGfez
via
logoblog

Thanks for reading Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Yatembelea Kiwanda cha ALAF.

Previous
« Prev Post