GWAMBINA YAJIMWAMBAFAI KUIFUNGA AFC

  Masama Blog      
 Timu ya Gwambina ya Misungwi ya Mwanza imejigamba kuifunga timu ya AFC ya Arusha kwenye mapambano mkali wa ligi daraja la kwanza utakaofanyika leo jumamosi ya Januari 18 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. 

Kocha wa Gwambina, Fulgence Novatus alisema wamejiandaa ipasavyo kuifunga AFC kama walivyowafunga mabao 3-0 walipocheza nao Mwanza. 

Novatus alisema Gwambina imeshazifunga timu kwao baadhi ya timu hivyo AFC watarajie kipigo jijini Arusha japokuwa hawajawahi kufungwa au kutoka sare jijini Arusha. 

"Timu za Mashujaa na Rhino zilikuwa hazijawahi kufungwa nyumbani kwao lakini sisi Gwambina tuliwafunga kwao hivyo AFC atarajie kipigo tena nyumbani kwao," alisema Novatus. 

Alisema vijana wake wana morali ya hali ya juu katika mpambano huo hivyo wanatarajia ushindi tuu bila wasiwasi wowote ule. 

Hata hivyo, kocha wa timu ya AFC Ulimboka Mwakingwe alisema anatarajia watashinda mpambano huo ili kulipiza kisasi kwa timu hiyo. 

Mwakingwe alisema AFC ya sasa siyo ile iliyofungwa mabao 3-0 na Gwambina kwenye mchezo wao wa awali.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30w9Iio
via
logoblog

Thanks for reading GWAMBINA YAJIMWAMBAFAI KUIFUNGA AFC

Previous
« Prev Post