Ticker

10/recent/ticker-posts

FFWPU yachangia Damu zaidi ya Uniti 1000


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TAASISI ya Mifupa (MOI), imekusanya zaidi ya Uniti 1000 za damu kutoka kwa wanachama wa Taasisi ya Familia ya Amani Duniani FFWPU kujitokeza kuchangia damu hiyo.

Uchangiaji wa damu umekuja ikiwa ni siku chache MOI kutangaza kuhitaji damu kutoka kwa wadau katika kuokoa maisha yawahitaji damu.

“Katika utoaji wa huduma hakuna mgonjwa aliyewahi kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu, tunauzoefu wa kuratibu wa kuwahudumia wagonjwa kwa kuhakikisha kunaupatikanaji wa damu katika taasisi na matumizi nyetu kwa siku ni chupa 16”amesema Mvungi

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msemaji wa MOI Patrick Mvungi amesema taasisi hiyo inauhitaji wa damu kwa ajili ya watu wanaofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo.

“Tulishirikiana na Shirika hili kutoa hamasa kwa wananchi na watu wengi wamejitokeza kwa idadi kubwa na kuvunja rekodi tangu kuanzishwa kwa taasisi hii”amesema Mvungi.

Patrick amesema katika utoaji wa huduma wamejipanga kwa kiwango kikubwa lakini changamoto kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa damu kutokana na mwitikio kama huu kutaongeza kutatua chanhgamoto hiyo.

Kwa Upande wake Kiongozi Mkuu wa kitaifa wa FFWPU Stylos Simba alisema waliamua kuonyesha moyo huo wa kuhamasisha wananchama wake kujitolea damu kutokana na changamoto ya damu iliyotangazwa katika taasisi hiyo.

“Baada ya kuonana na uongozo wa MOI niliwaahidi kuwa wanachama wetu zaidi ya 1000 kutoka Mbagala watakuja kuchangia damu “alisema.

Alisema hamasa hiyo ya wananchi imetokana na elimu waliyoitoa kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutoa mchango wa damu.

“Leo wanachama wetu kutoka mbagala wamekuja lakini tunawanachama wengi kutoka maeneo mengi watakuja hapa kuchangia damu ili kuunga mkono juhudi za serikali katika uimarishaji wa huduma za afya na pia wanachama wetu wengine wataenda kutoa huduma zingine za afya morogoro”Amesema Mvungi.

 
Picha mbalimbali za uchangiaji wa damu kwa wanachama wa Taasisi ya Familia ya Amani Duniani FFWPU katika Taasis ya Mifupa (MOI) jijini Dar es Salaam.
 



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30d8J6y
via

Post a Comment

0 Comments