DKT. NDUGULILE ATUMBUA WAWILI HOSPITALI YA TUKUYU

  Masama Blog      

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya jarada la mgonjwa katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Tukuyu wakati wa ziara yake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitazama dawa katika stoo ya dawa ya Hospitali ya Tukuyu wakati wa ziara yake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mfumo wa makusanyo wa mapato katika Hospitali ya Tukuyu wakati wa ziara yake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wagonjwa walikuwawakisubiri huduma ya X ray katika Hospitali ya Tukuyu wakati wa ziara yake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na mzee aliyekuwa akisubiri matibabu katika katika Hospitali ya Tukuyu wakati wa ziara yake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


…………….

Na Mwandishi Wetu Tukuyu Mbeya

*Asikitishwa na utoaji wa huduma za Afya Wilaya ya Rungwe

*Aaagiza uchunguzi wizi wa dawa katika vituo vya kutoa huduma za afya Mbeya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu Bw, Manase Ngogo na Afisa Ugavi Bi. Vumilia Mwaijande kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo Wilayni Rungwe mkoani Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Tukuyu na kujionea utendaji mbovu wa Hospitali hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Ndugulile amegiza kukatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa stoo ya dawa na kukosekana kwa taarifa sahihi za Dawa zinazotoka na zinazoingia katika stoo hiyo.

“Nilishapata taarifa za wizi wa dawa Tukuyu sasa hili linadhibitisha hilo, huwezi ukamuweka Afisa Ugavi asimamie stoo ya Dawa wakati Mfamasi yupo” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amesikitishwa na utendaji mbovu wa Hospitali hiyo usiozingatia maelekezo ya Wizara katika uendeshaji wa Hospitali katika maeneo tofauti ya utoaji huduma.

Dkt. Nduguile amewapa onyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, muuguzu Mkuu wa Wilya na Mfamasia wa Hospitali na kuwataaharalisha na utendaji wao wa akzi kwani umekuwa sio wa kuridhishwa na ameahidi kuwangalia kwa karibu zaidi.

“Katika ziara zangu zote sijawahi kuona utumbo kama huu niseme tu sijaridhishwa na utendaji wenu kabisa na Mganga Mkuu wa Mkoa chukua hatua Wilaya ya Rungwe hatufanyi vizuri katika Sekta ya Afya tunamuangusha Mhe.Rais Magufuli” alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Mnkondo Bendera amesema kuwa kama Wilaya hawezi kuvumilia uozo wa watoa huduma za afya kwani wataendelea kuangalia kwa karibu Sekta ya afya na watakaogundulika wanahujumu Sekta hiyo watachukuliwa hatua kali.

“Kwakweli hatuvumiliahaya kama ninyi wasaidizi wetu katika Sektaya Afya mnambinu za kutuhujumu katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi basi tutawashughulikia ipasavyo” alisema Bw. Bendera.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30omvn0
via
logoblog

Thanks for reading DKT. NDUGULILE ATUMBUA WAWILI HOSPITALI YA TUKUYU

Previous
« Prev Post