DKT. BASHIRU APOKEA MAPENDEKEZO YA ILANI KWA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI

  Masama Blog        Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amepokea mapendekezo ya Ilani ya mwaka 2020 – 2025 kutoka kwa Jumuiya ya Walemavu Nchini.Mapendekezo hayo yametolewa kwa wajumbe na wananchi wote wenye ulemavu kutoka kanda tisa nchini
Makabidhiano hayo yamefanyika jioni ya leo tarehe 30 Januari, 2020 Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Katika makabidhiano hayo, wajumbe wa Jumuiya hiyo wameishukuru na kuipongeza CCM na Serikali yake, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, kwa kuwajali na kuweka sera rafiki na wezeshi kiuchumi, kijamii na siasa ikiwa ni pamoja na kuwazingatia katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Jumuiya hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Ndg. Peter Sarungi akiwa na viongozi na wajumbe mbalimbali.Huu ni muendelezo wa CCM kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu kupokea mapendekezo mbalimbali kuelekea kuandika Ilani mpya Jumuishi ya Uchaguzi Mkuu kwa Mwaka 2020 – 2025, kutoka kwenye Taasisi, mashirika, vyama vya siasa na vya kijamii nchini, makundi ya wasomi na watu binafsi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36EnbWV
via
logoblog

Thanks for reading DKT. BASHIRU APOKEA MAPENDEKEZO YA ILANI KWA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI

Previous
« Prev Post