DC NDEJEMBI AAGIZA TARURA KUJENGA DARAJA LA MUDA KIJIJI CHA MSETO

  Masama Blog      

Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deo Ndejembi ameagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanajenga daraja la muda litakalowasaidia wananchi wa kijiji cha Mseta baada ya lile lililokuepo kusombwa na maji.

Wananchi wa kijiji hicho wameshindwa kuvuka kwenda ng'ambo ya pili yalipo makao makuu ya wilaya kufuatia mvua zinazonyeesha kwa sasa nchini kusomba daraja lililokuepo awali.

Adha hiyo ya kukosekana kwa daraja imesababisha wanafunzi kushindwa kwenda mashuleni huku ikihatarisha usalama wa wananchi hao endapo ikatokea mgonjwa mwenye kuhitajika kupelekwa Hospitali ya Wilaya.

DC Ndejembi amefika katika eneo hilo akiambatana na Meneja wa TARURA wa Wilaya na kumtaka kushirikiana na wananchi kujenga daraja la muda kabla ya kujenga daraja la kudumu pindi mvua zitakapomalizika.

Awali wakizungumza na Michuzi, Wananchi hao wameiomba Serikali kuwajengea daraja hilo kwani limekua likikwamisha maendeleo yao, kuhatarisha maisha yao na kukwamisha watoto kwenda shule.

" Nimefika hapa kujionea hali ilivyo lakini tayari nishamuagiza Meneja wa Tarura kujenga daraja la muda kabla hawajaanza kujenga daraja la kudumu pindi mvua zitakapomalizika.

Tunashukuru Serikali kuu chini ya Rais Magufuli kwa kutuletea kiasi cha Sh Milioni 270 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu ambalo litakua mwarobaini wa changamoto hii. Niwatake wananchi kuwa watulivu ndani ya muda mfupi daraja la muda litakua limekamilika," Amesema Ndejembi.


Mkuu wa Wilaya Kongwa, Deo Ndejembi akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tarura wilaya juu ya kujengwa kwa daraja la muda litakalowasaidia wananchi wa kijiji cha Mseta kuvuka kwenda upande wa pili.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akiwa kwenye eneo ambalo daraja limesombwa na maji na kusababisha wananchi kushindwa kuvuka kwenda upande wa pili.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akiwa na Katibu Tawala Wilaya (kulia), na watalaamu kutoka TARURA wakikagua maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mvua wilayani humo.  

Eneo ambalo daraja limesombwa na maji kwenye kijiji cha Mseta wilayani Kongwa na kusababisha wananchi kushindwa kuvuka upande wa pili. Kwa mbali ni wanafunzi wakiwa wameshindwa kuvuka. 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38iKNlo
via
logoblog

Thanks for reading DC NDEJEMBI AAGIZA TARURA KUJENGA DARAJA LA MUDA KIJIJI CHA MSETO

Previous
« Prev Post