DC KATAMBI AJA NA MBINU YA KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAJILI WA LINE ZA SIMU DODOMA

  Masama Blog      
Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha kila Mwananchi anasajiliwa line zake za Simu Wilayani Dodoma kwa kuzingatia agizo la Mhe. Rais Dk Magufuli, Mkuu wa Wilaya hiyo ameziagiza Taasisi zote ambazo zinashughulikia zoezi hilo la usajili kwa njia ya vidole kuhakikisha wanatenga eneo la Nyerere Square kufanyia shughuli zao zote hapo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wao.

" Nimetembelea maeneo mengi ambayo watu wanasajili line zao za Simu kwa njia ya vidole na kujionea changamoto kadhaa hivyo naagiza watu wa NIDA, Uhamiaji na Makampuni ya Simu kuhamishia ofisi zao kwa muda ndani ya eneo la Nyerere pale ambapo wananchi watakua wanamaliza mambo yote hapo badala ya kutoka NIDA kisha aende Uhamiaji atoke Uhamiaji aende kusajili line badala yake vyote atavikuta hapo hapo," Amesema DC Katambi.

Ameagiza zoezi hilo kufanyika ndani ya siku mbili za Jumanne na Jumatano au siku nyingi zaidi ya hizo ili kuendana na spidi ya kuwawezesha wananchi kusajili line zao hizo huku akisema litawarahisishia huduma wananchi ambapo wataweza kumaliza kwa haraka na kuendelea na shughuli zao za kujenga Nchi.

Zoezi la kusajili line za Simu kwa njia ya vidole lilisogezwa mbele hadi Januari 20 mwaka huu na Mhe Rais Dk John Magufuli ili kuwapa nafasi wananchi ambao hawakua wamekamilisha zoezi hilo kuweza kukamilisha na baada ya hapo ambao watakua hawajasajili line zao zitafungwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi (mwenye suti nyeusi) akikagua zoezi la usajili wa line za Simu kwa njia ya vidole.
 Mkuu wa Wilaya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akikagua zoezi la uchukuaji wa vitambulisho vya Taifa NIDA kwa wananchi wa Wilaya yake kwa ajili ya kuweza kusajili line zao kwa njia za vidole.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akifuatilia zoezi la usajili wa line za Simu kwa alama za vidole jijini humo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2FFVt14
via
logoblog

Thanks for reading DC KATAMBI AJA NA MBINU YA KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAJILI WA LINE ZA SIMU DODOMA

Previous
« Prev Post