ASTON VILLA WAMTAMBULISHA RASMI SAMATTA

  Masama Blog      
Klabu ya Aston villa imekamilisha uhamisho wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Genk na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania  Mbwana Samatta (27) kwa makubaliano ya dau la £10m.

Samatta ametambulishwa rasmi  leo na klabu hiyo akiingia kandarasi ya miaka minne  na nusu mkataba utakaoishia July  2024.

Amesema, anafurahi kucheza Ligi Kuu ya Uingereza  kwani watanzania wengi wamekuwa wanatamani kuona wachezaji wao wanacheza kwenye Ligi hiyo.

Amesema, anaifahamu Aston Villa kwa kuwa amekuwa anaifuatilia kwenye Ligi Kuu Uingereza pamoja na wachezaji waliokuwa wanacheza hapo katika Kipindi cha nyuma hadi sasa.

Mshambuliaji huyo, anaenda kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji baada ya  kumpoteza mshambuliaji wa Brazil Wesley kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia na jeraha la goti alilopata katika mechi dhidi ya Burnley wakati wa siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Samatta alisajiliwa na Genk 2015 akitoka Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo ambapo amedumu katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minne akifungia timu yake magoli 76 katika michezo 191  akitoa na pasi za magoli 20.

Katika historia ya soka nchini, Samatta anakuwa Mtanzania wa Kwanza kucheza Ligi Kuu ya Uingereza na kuendelea kuweka historia na alama kwenye mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30CvIs8
via
logoblog

Thanks for reading ASTON VILLA WAMTAMBULISHA RASMI SAMATTA

Previous
« Prev Post