Ticker

10/recent/ticker-posts

ALIYEKUWA KIONGOZI WA BRIGEDI YA FARU APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA JESHI NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA

 Aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi leo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia) wakati alipofika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwaajili ya kuaga mara baada ya kuhamia Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru(kushoto) na aliyepembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi mara baada ya kukutana na aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) ambaye alifika katika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru na aliyepembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.
Aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru na kuhamia Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (wa pili kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (wa tatu kutoka kushoto) , Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Maafisa wa Jeshi la Wananchi mara baada ya kumalizika mazungumzo ya aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru Bregedia Jenerali Sibuti kuagana na uongozi wa Mkoa wa Tabora .

Na Tiganya Vincent, Tabora
ALIYEKUWA Kiongozi wa Brigedi ya Faru amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Jeshi la Wananchi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na aliyekuwa kiongozi katika Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti wakati wa mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alipofika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhama Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma.

Alisema katika kipindi alipokuwa akisimamia Brigedi ya Faru, Jeshi la Wananchi limeweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira na upandaji miti katika kutekeleza agizo la Makamu wa Rais.

Brigedia Jenerali Sibuti aliongeza kuwa ana matumaini Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi yake ya kuongoza Brigedi ya Faru ataendelea ushirikiano uliopo na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alimshukuru Brigedia Jenerali Sibuti kwa mchango wake mkubwa wa kukuza ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi na Mkoa wa Tabora na kusaidia katika upandaji miti kwa kutumia wanajeshi.

Naye Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru alisema Jeshi la Wananchi litaendelea kuunga mkono juhudi za uongozi wa Ofisi ya Mkoa wa Tabora ya kuugeuza Mkoa huo kuwa wa kijani kwa ajili ya kukabiliana na uharibifu wa mistu.

Alisema ataendelea kutoa Vijana wa Jeshi la Wananchi ili waweze kushiriki katika upandaji wa miti na shughuli nyingine za maendeleo kwa ustawi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2TkAxVm
via

Post a Comment

0 Comments