Ticker

10/recent/ticker-posts

WiLDAF yasema rushwa ya ngono bado tatizo makazini

RUSHWA ya ngono sehemu nyingi za kazi bado ni tatizo nchini hivyo wafanyakazi wameshauriwa kufichua vitendo hivyo ili waweze kupata msaada wa kisheria na wahusika kuchhukuliwa hatua.

Hayo yamesemwa jleo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) Anna Kulaya alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili baina ya shirika hilo na viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi kuhusu ukatili na unyanyasaji wa kijinsia sehemu za kazi.

Amesema sehemu ya kazi inapaswa kuwa salama kwa mfanyakazi kwani ni sehemu ambayo mfanyakazi anachukua muda mrefu kuishi.“Kuna ukatili mkubwa sehemu za kazi, na kwa kuwa nyinyi ni viongozi sehemu zenu za kazi mtakuwa mnajua zaidi kuliko sisi, hivyo tumewaita hapa siyo kutafuta mchawi bali kutafuta namna ya kutokomeza hali hiyo,” amesema Kulaya.

Amesema mwaka jana alituma timu ya wafanyakazi wake kwenda kuzungumza na wafanyakazi sehemu mbalimbali za kazi na walichokuta huko kinasikitisha sana kwani wafanyakazi kwenye sehemu mbalimbali walizungumza kwa uwazi kuhusu rushwa ya ngono sehemu za kazi na ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa hasa wanawake.

“Tulichoona huko ndicho kimetusukuma kuandaa mdahalo wa leo baina yetu ili tujadiliane na tuangalie namna ya kuweka mifumo ambayo itakuwa na msaada mkubwa wa kukabiliana na hali hii,” amesema Mkurugenzi Kulaya.

Naye, Mwajina Lipinga kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi alisema serikali iliamua kuanzisha Mpango wa Kutokomeza Ukatili wa Wanawake na Watoto MTAKUWWA baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya.Amesema wakati wa mchakato wa kuanzisha mpango huo wadau mbalimbali walijitokeza wakiwemo WiLDAF ambao wamekuwa bega kwa bega na serikali katika utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kufikia lengo mwaka 2022.

“Serikali iliona kuna shida kubwa kwenye ukatili hasa wanawake na watoto na lengo la MTAKUWWA ni kutokomeza ukati kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50 ikiwezekana kutokomeza kabisa,” alisema
Alisema maeneo ya umma na ya kazi si salama sana kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanyika hivyo wadau hao wananafasi kubwa ya kuzuia na kumaliza vitendo hivyo.
 : Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo (Afrika) WiLDAF Anna Kulaya akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na vyama vya siasa kuhusu usalama sehemu za kazi na masuala ya ruhwa ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia.
Viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi na vyama vya siasa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika WiLDAF alipokuwa akifungua mkutano wa kujadili usalama sehemu za kazi jijini Dar es salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35IAvKs
via

Post a Comment

0 Comments