WAZIRI BASHUNGWA AWAAGIZA WATUMISHI WA WIZARA YAKE NA TAASISI ZAKE KUSOMA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

  Masama Blog      
Ninamuagiza kila mtumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake kuhakikisha anasoma hotuba aliyotoa Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ya tarehe 12, Disemba 2019 kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya taifa (HKT) ya CCM uliofanyika mjini Mwanza.

Hotuba imesheheni dira, fikra na maono ambayo utekelezaji wake utaleta mageuzi makubwa ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu na wanachi wake kufikia mwaka 2030.

Kwa muktadha huo, Wizara inafanya zoezi la kuhakikisha sera na mipango mikakati yake yote inafanyiwa mapitio ili kuongeza weledi na wigo wa Wizara kuendelea kuratibu suala zima la ujenzi wa uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.

Tanzania ya viwanda inazidi kuonekana. Watanzania Tumemuelewa Rais wetu Magufuli, vision na political leadership yake ya kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini. Watanzania tumeamua kutokurudi nyuma. Mashambani, viwandani, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara, wajasiriamali tuchape kazi. Tushike neno tutende neno ili mageuzi haya yalete heri kwenye kila kaya nchini.

By. Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara.
Dec 16, 2019


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36Bpaf9
via
logoblog

Thanks for reading WAZIRI BASHUNGWA AWAAGIZA WATUMISHI WA WIZARA YAKE NA TAASISI ZAKE KUSOMA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Previous
« Prev Post