Ticker

10/recent/ticker-posts

WATOTO WENYE UHITAJI WAKARIBISHA SIKUKUU YA KRISMAS KIMICHEZO


    Na.Khadija seif, Michuzi TV

MLEZI wa kituo cha kulea watoto yatima cha kurasini Bi.Anna amewaomba wazazi kuiona fursa ya kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu

Bi.Anna amesema hayo wakati wa sherehe ya kukaribisha sikukuu ya krismas iliyoandaliwa na hoteli ya serena jijini Dar es salaam na kujumuisha watoto yatima kutoka vituo mbalimbali .

"Watoto hawa ni wetu sote jukumu la kuwalea sio la serikali au watu binafsi peke yao bali ni jukumu la Kila mtanzania kwani tukiwaacha  tunawatengenezea mazingira hatarishi na kupelekea kujiingiza kwenye vitendo viovu vya ubakaji,ukahaba pamoja wizi na kusababisha nchi kuwa na watu waovu wengi na kurudisha maendeleo ya jamii yetu kuzorota"

Aidha,mama mlezi wa watoto ameeleza changamoto anazopitia katika ukuaji wao hasa wale walemavu ni pamoja na kukosa vifaa vinavyowawezesha kufanya mawasiliano ya usiku kwa viziwi, na baiskeli kwa watoto walemavu wa miguu.

"Kuelekea sikukuu ya Christmas na sikukuu nyingine watu wamekua wakija kituoni na kuwapatia misaada mbalimbali watoto wetu kuonyesha upendo na jinsi gani wanawathamini watoto ,"

Pia amewapongeza uongozi wa hoteli ya serena kwa kuendelea kuonyesha upendo wa dhati kila mwaka na kuwakaribisha watoto na kucheza,kujumuika kwenye chakula pamoja nao.

''watoto wanapokutana na kushiriki michezo inawajengea uwezo wa kujiamini mbele za watu na pia inatupa uhalisia kuwa hata wao wanavipaji vingi na hasa leo tumeona wengi wanajua kuimba na kucheza,"
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35UrIF1
via

Post a Comment

0 Comments