Wataalam wajengewa uwezo kupunguza vifo kwa watoto wanaozaliwa utumbo nje

  Masama Blog      
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza, Dkt. Naomi Wright akielekeza namna ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa matumbo yakiwa nje.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zaituni Bokhari akielezea kwa vitendo namna ya kutumia mfuko safi wa plastiki ili kuzuia upotevu wa maji maji na joto la mwili kwa mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje kabla ya kumpeleka katika hospitali yenye wataalam bobezi.
 Wataalam wa Afya wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa hospitalini hapa leo.
 Daktari wa Watoto MNH, Dkt. Neema Bayyo akionyesha jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje.
 Dkt. Zaituni Bokhari akishirikiana na Dkt. Neema kuhifadhi matumbo yaliyotoka nje kwa kutumia mfuko maalum (Silo bag).
Dkt. Bokhari na Dkt. Wright wakielekeza namna mama anavyotakiwa kumbeba mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje mara baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.


Wataalam wa Afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo wamejengewa uwezo ili kuwasaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje.

Ambapo takwimu za Hospitali ya Taifa  Muhimbili zinaonyesha kuwa asilimia 100 ya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje hupoteza maisha kutokana na ukosefu wa elimu kwa watoa huduma za afya ya namna wanavyoweza kutoa huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha mtoto katika hospitali zenye wataalam bobezi.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zaituni Bokhari wakati wakutoa mafunzo hayo kwa njia ya vitendo yanayolenga kuwafikia watoa huduma za afya katika hospitali mbalimbali za rufaa ndani na nje ya Dar es Salaam.

“Tunatumaini kuwa mafunzo haya yatasaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje ambapo hadi sasa tayari madaktari na wauguzi wa MNH-Upanga na Mloganzila wamekwisha kupatiwa mafunzo na kuanzia kesho tutaanza kuzifikia hospitali mbalimbali za rufaa ndani na nje ya Dar es Salaam ili kuwapatia mafunzo haya,” amesema Dkt. Bokhari.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza, Dkt. Naomi Wright ametaja nchi nne ambazo zimechaguliwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa watoto hao kuwa ni Tanzania, Ghana, Zambia na Malawi.

“Sababu hasa ya Tanzania kupatiwa mafunzo haya ni kutokana na ongezeko la vifo vya watoto wanaozaliwa matumbo yakiwa nje ambapo kwa nchi zilizoko kusini wa jangwa la Sahara ni zaidi ya asilimia 98%,” amesema Dkt. Wright.
Baadhi ya mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na jinsi ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje, njia sahihi za kutoa huduma kwa mtoto huyo kwa kutumia mifuko safi ya plastiki na hatua za kufuata wakati wa kujiandaa kumtoa mtoto katika hospitali aliyopokelewa hadi kumfikisha katika hospitali yenye wataalam bobezi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PQlS0N
via
logoblog

Thanks for reading Wataalam wajengewa uwezo kupunguza vifo kwa watoto wanaozaliwa utumbo nje

Previous
« Prev Post