Ticker

10/recent/ticker-posts

Wapongezwa kwakufanya mapitio ya Sera ya afya

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ameipongeza wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto kupitia idara ya maendeleo ya jamii kwa kuona umuhimu wa kufanya mapitio ya sera yake ili kupata sera iliyo shirikishi.

Ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua kikao kazi cha mapitio ya sera ya maendeleo ya jamii kwa kanda ya Kaskazini katika mkoa wa Arusha ambacho kikao hicho kilijumuisha mikao ya Kilimanjaro, Tanga na Manyara.

“Ni vizuri kufanya mapitio ya sera hii ili iweze kuendana na hali halisi ya sasa hasa katika serikali hii ya viwanda katika uchumi wa kati kwa kugusa makundi ya watu mbalimbali kama walivyo katika kikao hiki”.

Kwitega amesema dunia imebadilika na mambo mengi yamebadilika hivyo hata pia sera zetu zinapaswa kubadilika kulingana na mabadiliko haya hasa kwenye maswala ya wanawake na watoto.

Hivyo amewataka wadau wote walioshirikishwa kwenye kikao hicho kutoa maoni yao ili kuwezesha kupata sera iliyobora na inayogusa takribani kila eneo linalomgusa mwananchi wa hali yoyote.

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya maendeleo ya jamii Grace Magwa amesema, lengo kubwa la kikao hicho ni kupitia sera ya maendeleo ya jamii ya mwaka 2000 ili ieleweke kwa wadau wakikao.

Amesema, kisha wataitaji maoni kutoka kwa wadau hao katika kuboresha sasa sera inayokuja na akasema ndio maana wamepita katika kanda zote 7 zinazojumuisha mikao yote 26 ya Tanzania bara ili kutoa nafasi kwa wawakilisha wa makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Amesisitiza kuwa maoni hayo yatakuwa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kuwa na sera inayoendana na hali ya mabadiliko ya sasa ambayo yapo katika mabadiliko ya hali ya mazingira, afya na maeneo mengine mengi hivyo sera nayo inaenda kuzingatia mabadiliko hayo.

Bi Mariam Mollel kutoka baraza la wafugaji Mkoa wa Manyara amesema, bado kuna unyanyasaji mkubwa kwa wanawake katika kumiliki mali na kutoa maamuzi katika jamii nyingi hasa za kimasai,hivyo kwa mapitio ya sera hiyo itasaidia kuongeza vipengele vitakavyowezesha mwanamke kuepukana na changamoto hiyo.

Kutokana na mabadiliko mbalimbali katika jamii nyingi za Kitanzania, wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto imeamua kufanya zoezi la kupitia na kukusanya maoni juu ya sera ya mwaka 2000 yenye mkakati wake wa mwaka 2015 ambayo nayo ilirekebishwa kutoka katia sera ya mwaka 1992 ili kupata sera bora na shirikishi kwa miaka ijayo ambapo makundi mbalimbali yalishirikishwa yakiwemo viongozi wa dini, watalaamu, taasisi binafsi,  na vyama mbalimbali vya kijamii.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38XXqTQ
via

Post a Comment

0 Comments