DOWNLOAD APP YETU HAPA

WANANDOA WAKONGWE DUNIANI WAELEZA SIRI YA MAFANIKIO YAO

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAKIWA na jumla ya miaka 211 John (106) na Charlotte  Henderson (105)Desemba 15 wataadhimisha miaka 80 ya ndoa yao huku wakieleza siri ya mafanikio yao ni kutengeneza kesho bora zaidi kuliko leo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Guinness World Record imeelezwa kuwa wanandoa hao waishio Texas nchini Marekani walikutana mwaka 1934 katika Chuo cha Texas ambapo Charlotte alikiwa akisomea masuala ya elimu na John alikuwa mcheza mpira maarufu chuoni hapo.

Licha ya kutobahatika kupata mtoto wawili hao wameeleza kuwa siku zote wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali  Kama vile kucheza pamoja na kufanya mazoezi.

Charlotte amemwelezea mumewe John kuwa ni mwelewa sana na mwenye moyo wa kusamehe;

"Hatukumbushiani mambo yaliyopita baada ya kusamehe, tunaishi kwa furaha na mapenzi ya hali ya juu" ameeleza.

Kwa upande wake John amemwelezea mkewe kuwa ni mwanamke anayejali na wamekuwa wakizidi wakifurahia kila siku.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33EN8nY
via
logoblog

Thanks for reading WANANDOA WAKONGWE DUNIANI WAELEZA SIRI YA MAFANIKIO YAO

Previous
« Prev Post