Wakulima Wa Tumbaku Kaliua Watakiwa Kuanzisha Mashamba Ya Miti

  Masama Blog      
Na, Editha Edward -Tabora.
 
Wakulima wa zao la Tumbaku wilayani Kaliua Mkoani Tabora wametakiwa Kuanzisha Mashamba ya Miti ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika vijiji vyao 

Ametoa Agizo hilo mkuu wa wilaya hiyo Abel Busalama wakati akizindua kampeni ya upandaji  Miti kwa Wakulima wa Tumbaku ndani ya wilaya hiyo 

Amesema Miti ni muhimu kwa sababu inachochea uwepo wa mvua unasababisha udongo uwe na rutuba pamoja na kutunza uoto wa asili 

Pia amesisitiza ili kunusuru mazingira kutokana uharibifu mkubwa unaochochewa na ukataji Miti kwa ajili ya shughuli za   kilimo hivyo Kila mkulima anatakiwa kupanda Miti katika mashamba yake

Busalama pia ameagiza Wakulima wote wanaolima zao hilo kununua mashamba na kupanda Miti ya kutosha ili kuhamasisha makampuni yanayonunua zao hilo kuongeza idadi ya kilo watakazonunua 

Aidha amesema wataanzisha msako wa kukagua Kila shamba Kama Miti hiyo itapandwa na endapo kwenye shamba atakapokutwa hajapanda Miti atachukuliwa hatua ikiwemo kuzuiwa kupima hadi atakapopanda Miti 

Katika hatua nyingine ameipongeza kampuni inayonunua zao hilo la Tumbaku wilayani humo ya Japan Tobacco International (JTI)  kwa kusimamia ipasavyo kampeni ya uanzishaji mashaba ya Miti kwa vyama vya Wakulima wa Tumbaku katika wilaya hiyo

Kwa upande wake Ofisa wa JTI Chrispin Mchafu amesema kampuni hiyo imeanzisha kampeni ya upandaji Miti kwa vyama vyote vya Wakulima wa zao hilo na  kuongeza uzalishaji wa Tumbaku.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima. 
Pichani ni baadhi ya wakulima wa Tumbaku wilayani Kaliua Kila mmoja akiwa ameshikilia mche wa mti ili kwenda kupanda mashambani mwao.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Z6Zg0k
via
logoblog

Thanks for reading Wakulima Wa Tumbaku Kaliua Watakiwa Kuanzisha Mashamba Ya Miti

Previous
« Prev Post