WAHITIMU WA VYUO MBALIMBALI WAASWA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU

  Masama Blog      
Na Pamela Mollel, Arusha

Wahitimu waliohitimu katika vyuo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutojihusisha na aina yeyote ya uhalifu Jambo ambalo litapelekea kuharibu malengo yao ya baadae

Akizungumza katika mahafali ya 21 katika chuo cha uhasibu Njiro Arusha hivi karibuni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adv.Fancy  Nkuhi aliwasihi wahitimu kutojiingiza katika uhalifu wowote

Alisema kuwa wapo baadhi ya wahitimu hujiingiza hata katika mitandao ya kijamii na kuanza kutukana serikali au hata watu mbalimbali

"Jamanii ukiangalia vizuri hawa wanaotukana watu hovyo pamoja na serikali hiyo ni hasira na walishindwa kuchukua hatua baada ya kuhitimu na nini kinafata na nini afanye ili kutimiza ndoto zake au malengo"Alisema Adv.Nkuhi

Pia aliwajulisha wahitimu hao kuwa safari ya mafanikio siyo rahisi Kama ambavyo wanachukulia, tena kwa kijana ni safari iliyo na mabonde mengi

"Maisha yanahitaji kujituma na kujitoa,vijana wengi sasahv hawataki kujitoa wanataka kulipwa fahamu kuwa unapojitoa ndipo unajijengea uzoefu mkubwa utakaokuwezesha wewe kuwa na mtandao,yaani kujulikana na watu hii itasaidia wewe kupiga hatua Kila siku"Alisema Adv.Nkuhi

Hata hivyo aliwataka wanafunzi kujua kuwa hapo hapo walipofika ni juhudu za wazazi wao hivyo wasiwaangushe bali kuchangamkia fursa zilizopo

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof.Eliamani Sedoyeka aliwataka wahitimu hao kuendelea kujifunza mambo mapya kwa kujiwekea utaratibu wa kusoma vitabu hali itakayosaidia kujiongezea maarifa mapya

Alisema kuwa ni vizuri wakajiwekea desturi ya kujiandaa kabla ya kufanya jambo lolote hiyo itasaidia kufanya vizuri zaidi

"Sisi Kama wasimamizi wenu tunatarajia maarifa na ujuzi mlioupata hapa mtumie katika kuwatumikia watanzania wote kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli"alisema Prof.Sedoyeka

Naye mtangazaji maarufu wa redio cloud's Meena Ally ambaye alikuwa mhamasishaji kwa wahitimu,Alisema kukata tamaa ndio dhambi kubwa inayowaangusha vijana wengi

"Mimi nilianza Kazi ya utangazaji nikiwa na umri mdogo wapo walioniona siwezi kutokana na umri lakini kwa vile nilikuwa napenda kazi ya utangazaji nilijituma kutimiza ndoto zangu bila kujali mazingira niliyokuwa nayo kwa wakati huo"Alisema Meena Ally
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adv.Fancy Nkuhi akiongea katika wahitu wa chuo cha Uhasibu Njiro katika mahafali ya 21 ya idara ya usimamizi wa Biashara,ambapo na mambo mengine aliwataka wahitimu kujiepusha na uhalifu wowote utakaopelekea kuharibu maisha yao.
 Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka akizungumza na wahitimu ambapo amewataka kutumia maarifa na ujuzi waliyoupata katika kuwatumikia watanzania wote katika kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli
 Mtangazaji maarufu wa redio cloud's Meena Ally ambaye alikuwa kama mhamasishaji kwa wahitimu akizungumza kwenye mahafali hayo huku akijitolea mfano kwa namna alivyopambana kutimiza ndoto zake bila kujali mazingira aliyokuwa nayo kwa wakati huo

 Rejina Charles ni mhitimu ambaye alishika nafasi ya kuwa mwanafunzi bora ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya Posta
 Mhitimu Boniface Nkaina  ni mwanafunzi bora ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya posta
 Samira Mohamed katika picha ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya posta
 Sehemu ya wahitimu wakiwa na nyuso za furaha.
Sehemu ya wahitimu


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36CqRsE
via
logoblog

Thanks for reading WAHITIMU WA VYUO MBALIMBALI WAASWA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU

Previous
« Prev Post