Ticker

10/recent/ticker-posts

VIONGOZI NDIO CHANZO CHA MAKUNDI YA CCM ARUSHA Inbox x

Na Woinde Shizza,Arusha 
  
Makundi yaliopo ndani ya chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha yanasababishwa na baadhi ya viongozi ambao sio waadilifu katika chama hicho mkoani Arusha
 
Hayo yameelezwa na katibu wa Itikadi na Uenezi taifa Wa chama cha mapinduzi  Hamphrey Polepole  ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha wakati akiongea na wajumbe Wala chama cha mapinduzi mkoa Wa Arusha wakati katika mkutano maalumu Wa uchaguzi Wa Mwenyekiti Wa CCM mkoa ambapo alisema kuwa makundi yaliopo ndani ya chama hicho yanasababishwa na baadhi ya viongozi Wa serikali na chama wasio waadilifu 

Alisema wanachama Wa chama hicho hawana makundi  wala magenge ,ila baadhi ya viongozi ambao sio waadilifu,wasiotaka kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi, wanaoweka maslayi yao mbele badala ya maslayi ya chama ndio wanaunda makundi na kutengeneza magenge ya kuboma chama badala ya kujenga.

"Niwaombe  wana Arusha tuache makundi tukijenge chama chetu,tusikubali baadhi ya viongozi wasiokitakia chama chetu mema wakawatengenezea makundi ndani ya chama nataka kuona Arusha yetu ikiwa tulivu ,ikiendelea kuwa ya kijani,majimbo yote yakiongozwa na CCM ,na serikali ikiendelea kuendeshwa na chama chetu na hii italetwa na umoja wetu,na sio makundi ya wanachama au viongozi" alisema Polepole

Alibainisha kuwa yeye kama mlezi Wa chama hicho mkoa Wa Arusha hatamfumbia macho kiongozi yeyote au mwanachama ambaye ataendekeza ,au ataongoza kuunda makundi katika chama hicho ,kwani wanataka makundi yaishe ili chama hicho kiweze kuendelea kuongoza serikali na kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa CCM mkoa Wa Arusha  Zelothe Steven Zelothe alitoa massa 48 kwa viongozi pamoja na wanachama Wa chama hicho wale wenye makundi kuyavunja Mara moja kwani wasipofanya hivyo na wakabainika hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema kuwa  Kazi kubwa ambayo anaifanya nikukijenga chama cha mapinduzi mkoa Wa Arusha ,kuyafuta Makundi na makambi yote ambayo yapo ndani ya chama hicho ,kwani kwakufanya ivyo atajenga chama imara chenye wanachama imara watakayo weza kuilinda na kuiongoza nchi.

"Makundi na makambi yanaleta msuguano kwenye maofisi,kusengenyana   had I kupelekea kazi kitofanyika vizuri lakini Mimi sitakubali jambo hilo litokee kwakweli "Zelothe

Alibainisha amejipanga kushirikiana na idara zote za serikali,taasisi binafsi ,viongozi Wa dini ,wananchi wote bila kuchagua hali yake kiuchumi ,huku akisisitiza kuwa atawapa ushirikiano zaidi wanyonge  kwa kutatua kero zao,atasimamia na kutatua kero za wananchi  na hii itasaidia kuendelea kujenga chama hicho.

Naye kada Wa Ccm aliejitambulisha  kwa jina LA Tausi Swalehe alisema ni kweli wanachama Wachama hicho hawana makundi ila kunabaadhi ya viongozi ambao sio waadilifu ndio wanatengeneza makundi ndani ya chama hicho.

Alibainisha kuwa nivyema wakaacha Mara moja tabia hiyo na kuanza kuwa pamoja na kujenga chama kimoja kitakacho waletea wananchi maendele


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36NPsuJ
via

Post a Comment

0 Comments