Ticker

10/recent/ticker-posts

VIJANA WA KANISA LA ABC TABATA JIJINI DAR ES SALAAM WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO


Vijana wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mandela wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kwenda kutoa msaada kwa waathirika 20 wa mafuriko na wazee wasiojiweza wanaoishi mtaa huo wa jana. Kulia ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila.
Mkutano kabla ya makabidhiano wa msaada huo ukifanyika.

Vijana wa kanisa hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi sh.50,000 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mandela Yusuph Nyombi.
Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Mariam Rashidi. Kutoka kulia ni Wajumbe wa mtaa huo, Leonard Chalema na Tablisa Bushir.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Chande Shomari. Katikati ni Mjumbe wa mtaa huo, Tablisa Bushir.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Lusiana Mkono.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Piamaria John.
Vijana wa kanisa hilo, wakimkadhi msaada huo, Khadija Mussa kwa niaba ya Mme wake, Juma Mwengele.
Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Naomi Mlowe ambaye vitu vyake na chakula vilisombwa na maji.
Msaada huo ukitolewa kwa familia ya Hassan Mbega ambayo nyumba yao na vitu mbalimbali na chakula vilisombwa na maji. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila.
Msaada huo ukitolewa kwa familia ya Omari Issa ambaye ni mgonjwa.


Na Dotto Mwaibale

VIJANA wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam wametoa msaada kwa waathirika 20 wa mafuriko na wazee wasiojiweza wanaoishi Mtaa wa Mandela.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila alisema wameguswa kusaidia waathirika hao na sio mara ya kwanza kusaidia jamii katika eneo hilo.

" Kila wakati tumekuwa na desturi ya kusaidia jamii inayotuzunguka hapa kanisani na baada ya kutokea mafuriko na baadhi ya wananchi kubomokewa na nyumba na kusombwa kwa vitu vyao pamoja na chakula tukaona tuwafariji kwa kuwanunulia chakula na vitu vingine" alisema Ndabila.

Alitaja baadhi ya vitu walivyotoa kuwa ni unga wa sembe, mafuta ya kula pamoja na sabuni vyote vikiwa na thamani ya sh.900,000 ambazo zilitokana na kuchangishana na kupata ufadhili kutoka kwa muumini mmoja wa kanisa hilo anayeishi Marekani Tamari Mwakakonyole.

Mbali ya msaada huo Ndabila alitoa sh.50,000 kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mandela Yusuph Nyombi zilizotolewa na kanisa hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali katika ofisi ya mtaa huo.

Akipokea msaada huo Nyombi aliwashukuru vijana hao na Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila kwa msaada huo na kuwa kanisa hilo linatakiwa kuigwa na watu wengine.

" Kanisa lenu limekuwa likigusa maisha ya watu kiroho na leo sio mara yenu ya kwanza kutoa msaada kwa jamii nakumbuka umewahi kutoa msaada kwa yatima, wazee na hata katika ofisi yangu nilipoanza kazi mwaka 2015 mlitusaidia kutununulia vifaa vya ofisini hakika ninyi ni watu wenye upendo wa hali ya juu" alisema Nyombi.

" Napenda kukushukuru Baba Askofu na uongozi wote wa kanisa lako kwa moyo mliouonyesha kwa wahanga hawa wa mafuriko hakika unastahili pongezi kubwa Mungu akaifungue milango yenye heri kwako na timu nzima ya vijana walioguswa na kutoa msaada huu, mmetenda mambo makubwa mno hakika Mungu akawalinde kwa moyo huu mlionao wa kusaidia watu kila leo naamini atazidi kuwa bariki na kuwafungulia milango ya riziki hatuna cha kuwalipa ila yeye atawalipa" alisema Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo, Tablisa Bushir.

Akizungumza katika makabidhiano ya msaada huo Askofu, Flaston Ndabila alisema ili kuunga mkono jitihada za Rais Dkt.John Magufuli katika sekta ya elimu kanisa hilo kwa kusaidiwa na familia ya Fanuel Leonard itawasaidia kuwanunulia vifaa vyote vya shuleni wanafunzi 50 kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari ambao hawana uwezo kabla ya kuanza masomo mwezi Januari mwakani.

Alisema kazi inayofanyika hivi sasa ni kuwahakiki wanafunzi hao ili kubaini kama kweli hawana uwezo na wanahitaji msaada.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wenzake Mzee Chande Shomari alishukuru kanisa hilo kwa kuwapa msaada huo ambao umetolewa kwa wakati baada ya kuathiriwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha mwanzoni mwa wiki hii na kuharibu miundombinu ya barabara, nyumba na kusomba vitu vya ndani pamoja na chakula.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZlDd67
via

Post a Comment

0 Comments