Ticker

10/recent/ticker-posts

VIJANA AFRIKA WAMESHAURIWA KUPANDA MLIMA KILLIMANJARO

Wahamasishaji kutoka nchi za Zimbambwe ,Tanzania na Uganda wakishuka kutoka katika lango kuu la hifadhi ya Mlima Killimanjaro baada ya Safari ya siku sita ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya khamasishaji wa Kiafrika kupanda mlima huo na kutimiza agenda za Afrika tunayoitaka 2063.

Na Woinde Shizza, Globu  ya Jamii, Killimanjaro.

Vijana kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vikubwa vilivyopo barani Afrika kama njia ya kuunga mkono utalii wa ndani katika nchi zao na kutumia vivutio hivyo kama njia ya kuhamasisha umoja wa Afrika  na ushirikiano katika Nyanja muhimu za maendeleo ikiwemo fursa za Utalii.

Wakizungumza baada ya safari ya siku sita ya kuelekea kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wajumbe watatu kutoka nchi  za Uganda,Tanzania na Zimbambwe walisema kuwa licha ya Mlima huo kuwa katika orodha ya maajabu saba ya dunia na kuwa mlima mrefu kupita yote barani hapa lakini bado vijana wengi hawajatembelea mlima huo.

Emanuel  Motta  ni Muhamasishaji kutoka nchini Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Origin Trail alieleza kuwa lengo la kupanda mlima huo ni kuhamasisha vijana kutoka nchi zote 55 za bara la Afrika kupanda mlima huo kwa lengo la kutimiza agenda ya Afrika tunayoitaka 2063  pamoja na kutimiza malengo endelevu ya umoja wa mataifa.

“Mwakani May 2020 tutakua na tukio kubwa la vijana kutoka nchi zote za Afrika watapanda Mlima Killimanajaro hii ni fursa tunaomba vijana waungane na sisi ,wako watakaopanda kwa miguu na wengine watatumia baiskeli “ Alisema Motta

Mkurugenzi wa Great Africa Art Banner  kutoka Zimbambwe, Munyaradzi Muzenda alieleza kufurahishwa na vivutio vilivyoko katika mlima huo ambao mtu yeyote akifanikiwa kuupanda na kulifa kileleni ni ishara ya ushujaa na kuzishinda changamoto za upandaji wa mlima na maisha kwa ujumla.

Muzenda alisema kuwa wanahamasisha vijana kuchora bango kubwa la Afrika tunayoitaka na kupeleka mabango hayo katika kilele cha mlima huo.

Mkurugenzi wa Shirika la Sister Sister Organization  Ayaa Musuya kutoka nchini Uganda alisema kuwa Mlima huo utatumika kama kiunganishi kwa vijana wa bara la Afrika kwa kuwaleta pamoja na kuweka mpango wa pamoja na kutekeleza agenda za Afrika tunayoitaka.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2P5xFId
via

Post a Comment

0 Comments