Ticker

10/recent/ticker-posts

TANZANIA MBIONI KUPATA CHETI NCHI ZILIZOKIDHI VIGEZO VYA KUDHIBITI RASILIMALI MADINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo wakati wa kikao na wasalamu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya nchi zilizo katika kanda ya Maziwa Makuu walipokutana ili kuwasilisha matokeo ya tathmini waliyoifanya Nchini.
Katibu Mkuu Wa Madini Prof. Simon Msanjila akichangia hoja wakati wa majadiliano
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongoza Kikao na wataalamu waliofanya tathmini ili kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti ili kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza matakwa ya Nchi wanachama kwa kutokuruhusu rasilimali za nchi kutumika kuchochea maasi.

Na Nuru Mwasampeta, DSM

Imeelezwa kwamba Kabla ya kuisha Mwaka huu wa Fedha 2019/2020 Tanzania itakuwa imepata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi iliyokidhi Vigezo vya nchi zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini yakiwemo madini kutochochea machafuko kwa nchi wanachama za maziwa makuu.

Cheti hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kutoa vibali kwa wachimbaji, wauzaji na wasafirishaji wa Madini ya Bati (tin), dhahabu na Tangsten kuuza Madini hayo nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo tarehe 18 Desemba, 2019 jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kilicholenga kupokea ripoti juu ya tathmini iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa hayo. 

Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Naibu Waziri Nyongo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjila na wataalamu kutoka viongozi wa sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu yenye jumla ya nchi wanachama 12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali zinazopatikana katika nchi zao ili zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko katika nchi wanachama.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alisema anatarajia nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa pamoja ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo kutokana na nchi kukidhi matakwa muhimu ya kupewa cheti hicho.

Nyongo alisema kuwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieti Nchini kuanzia tarehe 13 hadi 18 Desemba, 2019 imeonesha wazi namna Serikali ya Tanzania inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo.

Akizungumza Namna mchakato wa tathmini hiyo ilivyofanyika, Gerard Nayuburundi mmoja kati ya wataalamu waliofanya tathmini nchini kutoka Burundi alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.

Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili Uwekezaji wao nchini kuwa na mtija.Akizungumzia namna tathmini hiyo ilivyofanyika Gerard alisema ilihusisha mahojiano na Ukaguzi wa taarifa mbalimbali wa namna mchakato wa uchimbaji, uuzaji, na usafirishaji wa rasilimali madini unavyofuata taratibu zilizowekwa na nchi wanachama.

Mpaka sasa ni nchi tatu tu za Uganda, Rwanda na Kongo zinazomiliki cheti hicho ambapo Tanzania itakuwa nchi ya nne kupewa cheti hicho muhimu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Mf2pG5
via

Post a Comment

0 Comments