TAMASHA LA MOYO WA IBADA KUFANYIKA KESHO VIWANYA VYA TANGANYIKA PACKERS JIJINI DAR

  Masama Blog      
 MKESHA wa Usiku wa Moyo wa Ibada kufanyika kesho katika viwanja vya Tanganyika Packers (Kawe), jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusifu na kuabudu kwa kumshukuru Mungu.

Akizungumza wakati wa kutambulisha tamasha la Mkesha huo, Mwimbaji wa Nyimo za Injili, Paul Mwangosi amesema lengo Kuu ni kuwakutanisha watanzania kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu na kusema asante kwa Ulinzi wa mwaka mzima  sambamba na kuliombea Taifa.

Amesema Tamasha linaandaliwa na huduma ya Moyo wa Ibada chini ya Mwimbaji wa nyimbo za Injili Paul Mwangosi ambaye ameimba nyimbo mbalimbali za kuabudu kama, Moyo wa Ibada, Nani kama wewe, Yesu Yesu, Nimesogea, Umeniosha bwana na nyingine nyingi.

"Tutakutana hapa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda mwaka mzima, tutaimba na kusifu sambamba na kupata neno la uzima lakini pia tutapata nafasi ya kusema neno kwa ajili ya nchi yetu. 


Amesema anatamani kila mmoja awe sehemu ya tamasha hilo na sehemu ya ibada hio kama ambavyo wakenya wamekuja kujumuika hapa nchini.

"Mwenyezi Mungu alituumba ili tumuabudu  kwani kumuimbia na kumsifu hata wanyama na mimea inafanya hivyo, ndio maana hatuchukulii kawaida kwa sababu imepangwa. Amesema Mwangosi.

Kwa Upande wake Mwimbaji kutoka Nchini Kenya, Sarah Mwangi,amesema unaweza kumwabudu Mungu kwa Kuimba, Kwa maombi, kwa kunena na kwakutabiri. Hivyo kila mmoja anakaribishwa katika viwanja vya  Tanganyika Packers.

"Ulimi unanguvu wa kunena mamo mazuri ambayo unataka kumlilia Mungu".


Tamasha hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 3 usiku hadi alfajiri ya kuamkia Desemba 14. Wahudumu wanaotarajiwa kuhudumu ni pamoja na Mwandaaji Paul Mwangosi,  Sarah Mwangi  Maarufu kama Sarah K.(Kenya) na Boaz Danken.
Muimbaji Paul Mwangosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkesha wa kusifu na kuabudu utakaofanyika Kesho Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers (Kawe),  jijini ar es Salaam. Kulia ni Mwimbaji, Gwamaka Mwakibete. Kulia ni Mwimbaji, Gwamaka Mwakibete.
Muimbaji wa Nyimbo za injili na kuabudu, Paul Mwangosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkesha wa kusifu na kuabudu utakaofanyika Kesho Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers (Kawe),  jijini ar es Salaam. Kulia ni Mwimbaji, Gwamaka Mwakibete, Kutoka kushoto ni Mwimbaji Jeremy Kitiku na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Sar mwangi maarufu kama Sarah K.
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya, Sara Mwangi marufu kama Sara K, katikati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkesha wa Kusifu na Kuabudu litakaofanyika Kesho Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers (Kawe),  jijini ar es Salaam. Kulia ni Mwimbaji wa nyimo za kuabudu, Paul Mwangosi na mwimbaji kushoto ni mwimbaji kutoka nchini Kenya Jeremy Kitiku.
Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya na hapa nchini wakiimba wimbo mojawapo utakaoimbwa hiyo kesho kwenye mkesha wa Kusifu na kuabudu


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36oFMGE
via
logoblog

Thanks for reading TAMASHA LA MOYO WA IBADA KUFANYIKA KESHO VIWANYA VYA TANGANYIKA PACKERS JIJINI DAR

Previous
« Prev Post