TAASISI YA WBM YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI YA SHULE YA MSINGU\I KIJITONYAMA

  Masama Blog      


Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Wezesha Binti na Mama aMjasiriamali (WBM) Latifa Mohamed akizungumza na wanafunzi wakati wa utoaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi 48 waliopata mafunzo ya ujasiriamali kutoka katika taasisi hiyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo ameipongeza Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananfunzi wa shule za Msingi na Sekondari.

WBM imetoa elimu kwa wanafunzi 48 wa Shule ya Msingi Kijitonyama waliopatiwa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na kupata vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, amesema taasisi ya WBM imeunga mkono jitihada za serikali katika kutoa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi na wamekuwa wa kwanza kuliona hilo hata baada ya serikali kurudisha mtaala utakaokuwa unafundisha fani mbalimbali. 

Amesema, unapompa mwanafunzi elimu ya ujasiriamali utamsaidia pindi atakapomaliza elimu yake iwe ya msingi au sekondari ataweza kiujiajiri na kuacha mawazo ya kuajiriwa kwani katika mwaka mmoja wanafunzi wengi sana wamekuwa wanahitimu elimu zao na wote wanasubiri kuajiriwa. 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijitonyama Beatus Amri ameishukuru taasisi ya WBM kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wanafunzi jambo ambalo litakuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yao ya baadae.

"Jambo hili ni kubwa sana nawashukuru WBM, wameona umuhimu wa kutoa elimu ya ujasiriamali wa wanafunzi hawa kwani hata sisi upo mtaala unaofundisha masuala mbalimbali ila kuja kwa wao ni chachu nyingine,"

Naye kwa upande wa Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya WBM Latifa Mohamed amesema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ilikua ni katika kumjenga mtoto wake na mama wa baadae kuacha fikra za kuajira na kutakiwa kujiajiri mwenyewe. 

Amesema, wamekuwa wanatoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, ambapo lengo likiwa ni kwa wanafunzi wa darasa la tano na sita na wale wa sekondari ambapo watapata mafunzi ya ujasiriamali na kupatuwa vyeti. 

Latifa ameeleza kuwa, kwa mwaka 2020 lego lao ni kuwaa na watoto 5000 kutoka katika shule za Msingi na Sekondari ambapo kila upande watachukua shule 50 kote nchini na sio Dar es salaam tu. Taasisi ya WBM wamelenga hususani kwa watoto wa kike ila waliona ni bora kutoa elimu hiyo kwa jinsia zote ambapo itawasaidia kujiajiri na kuacha fikra za kuajiriwa.
Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Wezesha Binti na Mama aMjasiriamali (WBM) Latifa Mohamed akiwapatia watoto vinywaji kabla ya kuanza zoezi la utoaji wa vyeti na zawadi.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akitoa zawadi kwa Mlezi wa Club ya WBM Mwalimu Margareth Mnyuko kama jitihada zake katika kuunga mkono mafunzo ayo waliyoyapata wanafunzi 48 wa shule ya Msingi Kijitonyama kutoka 
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama baada ya kuwakaidhi vyeti na tuzo ya kumaliza mafunzo ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama sambamba Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2P2zaXw
via
logoblog

Thanks for reading TAASISI YA WBM YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI YA SHULE YA MSINGU\I KIJITONYAMA

Previous
« Prev Post