TAASISI YA DIT YAASWA KUWEKA ATAMIZI KWAAJILI YA KUSAIDIA JAMII

  Masama Blog      


Katibu Mkuu- Mafunzo ya ufundi wa wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Avemaria Semakafu, akizungumza wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Preksedia Ndomba akizungumza wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.
Mmoja ya wafadhili wa tuzo na zawadi, Christopher Mgonja akizungumza na wanafunzi wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.
Mwenyekiti ya bodi ya Taasisi ya  Teknolojia Dar es salaam,profes Apollinaria akizungumza na wanafunzi wa DIT wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.Katibu Mkuu- Mafunzo ya ufundi wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Avemaria Semakafu, akiwakabidhi tunzo Baadhi ya wanafunzi bora wa Taasisi ya DIT  jijini Dar ea Salaam leo.

 TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), imeaswa kuweka atamizi ya wanafunzi wanaomaliza katika taasisi hiyo ili itokea uharibifu wa kompyuta katika taasisi z serikali waweze kuzitengeneza na si kutafuta mafundi wengine.

Katibu Mkuu-Elimu ya ufundi katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Avemaria Semakafu ameyasema hayo wakati akitoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika vitivo mbalimbali katika taasisi ya Teknolojia Dar ea Salaam (DIT) leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kompyuta zilizopo katika vyuo vya ualimu zimekaa kama mapambo kutokana na kuharibika.

"Tunakompyuta kibao katika vyuo vyetu vya ualimu lakini tunaambiwa sijui teknoloji gani imekosekana inahitajika kuzitengeneza programu ili ziweze kusoma, zimekaa kama mapambo. Kwahiyo kweli mnakuwa na atamizi hapa mtashindwa kwenda kututengenezea kweli. Kwa hiyo ninaomba nikualike mje mtufufulie kompyuta zile".

Avemaria amesema badala ya kwenda kutafuta fundi wa kutengeneza kompyuta mtaani, huko ni kuchezea fedha za walipa kodi.

Kwahiyo viundwe vikundi ambavyo vitasaidia kutengeneza kompyuta hizo.

"Kwahiyo mje mtusaidie kutengeneza kompyuta zetu".

Hata hivyo Semakafu amewashauri Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kuweza kushiriki moja kwa moja kanyika kuhakikisha kuunga mkono kazi za kibunifu zinazofanywa na wanafunzi wa taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), ziweze kuendelezwa.

Pia amewapongeza wanafunzi waliopata tuzo na zawadi, ni ishara ya kutambua na kuenzi juhudi kubwa wanazozifanya katika kujifunza na kuhakikisha wanafanya vyema katika mitihani na majaribio mbalimbali katika fani zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Preksedis Ndomba amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kupendekeza matatizo yanayoikumba jamii yao na kuyatatua. 

Ndomba amesema kuwa taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam inataoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri ili kuhamsisha juhudi na maarifa katika kushindana katika masomo wanayofundishwa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa bodi ya DIT,  Profesa Apollinaria amewapongeza walimu wanaowafundisha wanafunzi hao na mpaka kupata tuzo.

Mmoja ya wafadhidhi wa tuzo zilozotolewa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Chrostopher Mgonja amesema wanaamini kuwa vijana wote ni wazuri, na amewaomba vijana hao wakawe chachu huko wa endako na kuwafundisha wengine ili waweze kufaulu masomo yao.

"Tunacho waomba mkawe chachu huko mnakoenda na mjitahidi kuwatia moyo wenzenu ambao bado wapo hapa, naamini mnaweza mkawapa ujanja naweza kufaulu kwa namna gani".


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36t9PNG
via
logoblog

Thanks for reading TAASISI YA DIT YAASWA KUWEKA ATAMIZI KWAAJILI YA KUSAIDIA JAMII

Previous
« Prev Post