Ticker

10/recent/ticker-posts

SIMBA WAWILI WAUAWA KIJIJI CHA MATEPWENDE,WILAYANI NAMTUMBO



Na Yeremias Ngerangera….Namtumbo.

Simba wawili kati ya wanne wanaosumbua wananchi wa kijiji cha matepwende kata ya Msisima Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wameuawa kwa kupigwa risasi na mwananchi Omari Mtwalo Shekhe wa kijiji cha Matepwende kwa kushirikiana na askari wasaidizi wa wanyamapori wa kijiji hicho (VGS).

Mtendaji wa kata ya Msisima bwana Onesmo Mbiro alithibitisha kupigwa risasi simba hao muda wa saa nane mchana tarehe 11mwezi huu siku ya jumanne wakiwa wamejificha kwenye msitu uliopo jirani na mashamba ya wakulima.

Bwana mbiro aliongeza kuwa simba mmoja alipigwa na kufa hapo hapo lakini mwingine hakuweza kufia hapo badala yake alikimbia huku akiwa amejeruhiwa na asubuhi ya tarehe 12 alipatikana akiwa amekufa .

Fatuma Saidi mkulima wa mpunga wa kijiji cha Matepwende alidai wananchi wengi hawaendi shambani kwa hofu ya simba hao kwani bado simba wawili kuuwawa kwa kuwa walikuwa wanne katika kundi lao.

Fatuma alidai hofu ya wananchi hao iweze kuondoka ni mpaka pale itakapoonekana simba wawili wengine waliobaki wameuwawa machoni pa wananchi hao.

Tile Bashiru mkazi wa kijiji cha Matepwende alinusurika kuliwa na simba asubuhi na mapema wakati anaelekea shambani miezi mitatu iliyopita katika kijiji hicho na kuokolewa na umati wa wananchi baada ya yeye mwenyewe kupiga kelele kuhitaji msaada huku akiwa juu ya mti na simba wakiwa chini ya mti.

Bashiru alidai ni mungu aliyempa akili ya kuuparamia mti haraka wakati simba wale walipomwona na kutamani kitoweo na ndipo walipoanza kumkimbiza tile aliparamia mti uliokaribu kwa kuwa alifunuliwa na mungu kuwa hawezi kufika kokote na akili ikamtuma aparamie mti kwa haraka na kuwahi umbali mrefu hali iliyowshinda simba wale kufanya chochote baada ya kufika chini ya mti ule.

Wananchi walifurika na kwenda kumwokoa mwenzao na umati mkubwa wa watu ndio uliowafanya simba wale wakimbie katika eneo hilo na kumfanya tile anusurike kuliwa na simba hao.

Hata hivyo maafisa wanyama pori walihamia kijijini hapo na kupiga kambi lakini kwa mwezi zaidi ya mmoja simba hao hawakuonekana na badala yake maafisa wanyamapori waliacha silaha 2 aina ya raifoo katika ofisi ya kijiji na kumtaka shekhe Omari Omari Mtwala wa kijiji hicho kushirikiana na askari wasaidizi wa wanyamapori (VGS) kuendelea na doria kuwasaka simba hao ili wasilete madhara kwa wananchi.

Shekhe Omari Mtwala alisema kuwa alipatiwa taarifa na wananchi walioenda shambani asubuhi kuwa waliziona nyayo za simba katika maeneo ya mashamba yao na kuwafanya warudi shambani kwa hofu ya kuliwa na simba na ndipo yeye na askari wasaidizi wa wanyamapori wa kijiji walienda ofisi ya kijij na kwenda kuchukua silaha na kuelekea mashambani kulikoripotiwa kunekana nyayo za simba na kufanya doria.

Mtwala aliongeza kuwa wakati wapo kwenye doria ya kukagua nyayo za simba hao wakabaini wameingia kwenye msitu uliojirani na mashamba ya watu na wakaingia katika msitu huo kwa tahadhari kubwa na kuwaona simba hao wawili wakiwa wamelala pamoja na kuwamiminia risasi ambapo mmoja alikufa hapo hapo na mwingine alijivuta na kukimbia eneo hilo na leo tarehe 12 amepatikana amekufa.

Kijiji cha matepwende ni moja ya kijiji ambacho wananchi wake waliondolewa katika Hifadhi eneo la Ntanga lililokuwa na wanyama wengi na wananchi kuvamia eneo hilo kufanya eneo la Kilimo cha mpunga na kuondolewa mwaka 2017 na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Binilith Satano Mahenge kuwa eneo hilo ni Hifadhi ya wanyama na sasa wanyama wengi wanafurika katikaeneo hilo na kujitokeza katika makazi ya watu na kuleta hofu kwa watu wakihofia usalama wao.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38AK8fO
via

Post a Comment

0 Comments