Ticker

10/recent/ticker-posts

Serikali yalitaka Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kuendelea kutoa huduma za matibabu Kambi za Wakimbizi mkoani Kigoma


*******************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ametoa msimamo huo wa Serikali alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt. Mnyepe ameitaka UNHCR kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1991 hususani Ibara ya Pili na ya Tatu (Articles II & III). Ibara hizo zinaelekeza kwamba UNHCR ni lazima ishirikiane
 na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake hapa Nchini.

Hivi karibuni UNHCR ililitaka Shirika la Msalaba mwekendu Tanzania (TRCS) kukabidhi majukumu yao bila kuihusisha serikali. Hatua hiyo ya UNHCR inavunja makubaliano ya1991.

Hivyo amewaeleza UNHCR kwamba Shirika la Msalaba mwekundu Tanzania kuendelea na majukumu yake kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo mpaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNHCR watakapokubaliana vinginevyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ENXtUr
via

Post a Comment

0 Comments