Ticker

10/recent/ticker-posts

Serikali yaipa kipaumbele sekta ya michezo nchini kutoa ajira kwa vijana


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifunguamashindano ya pili ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akisalimiana naBalozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wamchezo wa Taekwondo kabla ya kufungua mashindano ya pili ya mchezo huo yanayofanyikakwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja waSheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wamchezo wa Taekwondo akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo Tanzania (TTF) Ramoudh Ally (kulia).
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea Taekwondo Cho Tae-ick (kushoto) akiteta jambo naNaibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kulia) wakati waufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanziatarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijiniArusha.
Rais wa Shirikisho la mchezo wa Taekwondo nchini (TTF) Ramoudh Ally akitoa historia ya mchezo wa Taekwondo nchini wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katikauwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ickWanamichezo wa mchezo wa Taekwondo wakiendelea na mashindano ya mchezo huo wakati wa ufunguzi wa mashindano yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha)
******************************
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha
Serikali ya Awamu ya Tano imeipa kipaumbele sekta ya michezo nchini kwa kuweka mikakati inayohakikisha michezo yote ikiwemo Taekwondo inafanya vizuri ili kuwa chanzo cha kutoa ajira kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa taifa.

Akifungua mashindano ya Taekwondo ya pili ya mchezo wa yanayofadhiliwa na Ubalozi wa Korea nchini kwa mwaka 2019 kwa nchi za Afrika ya Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mw wiki, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa michezo yote nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo.

Akijibu moja ya maombi yaliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo nchini (TTF) Ramoudh Ally la kupatiwa eneo la kujenga uwanja mkubwa wa ndani wa kisasa kwa ajili ya mchezo wa Taekwondo wakati akitoa historia ya mchezo huo nchini, Naibu Waziri alisemakuwa kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya michezo nchini ya mwaka 1995 jukumu la kusimamia na kuendeleza sekta ya michezo ni la Serikali, jamii nzima pamoja na wadaumbalimbali ukiwemo Ubalozi wa Korea nchini.

“Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendelea kushirikiana na Serikali kukuza, kuendeleza na kuwekeza katika sekta ya michezo nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo, kwani Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuendeleza michezo ikiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini ili kuhakikisha sekta hii inakuwa na tija kwa jamii na taifa zima” alisemaNaibu Waziri Shonza.

Aidha, ameataka maafisa michezo nchini kuanzia ngazi ya mikoa na wilaya kushirikiana na viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo ili kuhakikisha vyama na vilabu ambavyo havijapata usajili kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT) ambalo limepewa dhamana ya kusajilimashirikisho, vyama na vilabu hapa nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wa mchezo huo amesema kuwa mchezo wa Taekwondo unafaida nyingi na unachezwa na watu wa rika zote kuanzia watoto wadogo hadi watu wazima kwa kuimarisha na kujenga mwili ambapo husaidia kuimarisha umakini katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Balozi huyo ameendelea kuzitaja faida nyingine za mchezo huo kwa ni kuwajengea uwezo wachezaji wa kujilinda kiusalama, kuwafundisha saikolojia ya namna bora ya maisha pamoja na kuwajengea urafiki miongoni mwa wachezaji.

“Taekwondo ni mchezo mzuri sana, kila kitu katika mwili wa binadamu ni silaha ya kujikinga, cha msingi ni kujua namna ya kuitumia kwa faida kwa jamii nzima, elimu hiyo inapatikana katika mchezo wa Taekwondo” alisema Balozi Cho.

Awali akitoa historia ya mchezo wa Taekwondo nchini Rais wa Shirikisho la mchezo huo nchini (TTF) Ramoudh Ally alisema kuwa Taekwondo ni mmoja kati ya michezo inayotambuliwa na Baraza la Michezo Tanzania pamoja na Kamati ya Olympic duniani.

Mchezo Taekwondo nchini ulianza kutambuliwa rasmi mwaka 2003 na Shirikisho la Taekwondo duniani ambalo makao yake makuu yapo nchini Korea ya Kusini ambapo hadi sasa Tanzania ni mwanachama hai na inashughulika na masuala yote ya mchezo huo duniani.

Mashindano Taekwondo ya mwaka 2019 yanayojulikana kama “Korean Ambassador’s Cup” ni ya pili kufanyika nchini ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2017.

Mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14 hadi 15 Disemba 2019 jijini Arusha ambayo yanajumuisha jumla ya washiriki 172 kutokakatika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Uganda na mwenyeji Tanzania pamoja na washiriki kutoka nchini Malawi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38CNOxI
via

Post a Comment

0 Comments