SERIKALI YA ZANZIBAR KUHAKIKISHA LUGHA YA KISWAHILI INAIMARIKA

  Masama Blog      
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akifunga Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Ali Abeid Karume akizungumza katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili wakiwa katika ziara huko Bandarini Mjini Zanzibar.
PICHA NA MARYAM KIDIKO – MAELEZO ZANZIBAR.

***************************

Na Mwashungi Tahir Maelezo 20-12-2019.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha lugha ya Kiswahili inazidi kuimarika siku hadi siku kwa vizazi vya sasa na vijavyo ili viweze kufaidika.

Hayo ameyasema Waziri wa Nchi Afisa wa Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ufungaji wa kongamano la Tatu la Kiswahili la Kimataifa lililofanyika huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni .

Amesema lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inahitaji kukuzwa zaidi kwa wageni na wenyeji ili iweze kuwa mstari wa mbele katika kuzungumzwa ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema lugha ya Kiswahili haistahiki kubezwa kwani ni lugha inayothaminiwa na kuitaka jamii kuiendeleza na kuipa hadhi yake ya lugha hiyo kama lugha nyengine.

Hivyo alisema ni wajibu wetu kuithamini lugha ya Kiswahili na kuitumia katika matumizi sahihi kwani sie waswahili ni lazima kujivunia lugha yetu na sio nyengine bali ni Kiswahili.

Pia amesema Nchi nyingi duniani zinatumia lugha ya Kiswahili kufundishia katika vyuo vikuu na sehemu mbali mbali hasa ikiwemo Nchi ya Italia

Vile vile aliwataka waandishi chipukizi kutumia lugha ya Kiswahili ya ufasaha yenye kueleweka na kuwaiga waandishi wakongwe kama Shafi Adam Shafi ili kuiga kipaji chake na wao waweze kuendeleza mbele vipaji vyao.

Pia Balozi Seif alisema kuwa fursa ya Kiswahili ni hazina ya uchumi kujiongeza na kukidhi mahitaji maalum ya kibinaadamu na kuwataka jamii kuacha kuiga lugha za wenzetu.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili BAKIZA Amina AliKhamis akitoa maazimio ya Kongamano la tatu la Kiswahili amesema,Rais awe na mshauri wa masuala ya lugha, kujenga mshikamano zaidi kwa taasisi zinazounda istilahi na msamiati na wanahabari wa Kiswahili wawe wataalamu wa Kiswahili.

Kwa upande wa wageni walioshiriki kongamano hilo wamesema wamefaidika na mada zilizotolewa hapo na kuahidi watayafanyia kazi.

Aidha katika washiriki hao walipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za historia, bandarini, miti ulaya na kwahaji Tumbo ikiwa na lengo lake kuona sehemu alozitumia mwandishi mkongwe Shafi Adam Shafi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36Z6DJZ
via
logoblog

Thanks for reading SERIKALI YA ZANZIBAR KUHAKIKISHA LUGHA YA KISWAHILI INAIMARIKA

Previous
« Prev Post