Ticker

10/recent/ticker-posts

Programu ya Urithi Ukombozi wa Bara la Afrika ni ya Kimataifa


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akitoa maagizo wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kutafuta kuandaa maandiko ya kuomba ufadhili wa mradi huo pamoja na kuandaa mpango mkakati wa kutekeleza programu hiyo leo Jijini Dar es Salaam, alipotembelea Ofisi za Mratibu wa Programu wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, (katikati) ni Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akikagua hali ya Jengo ndani lilokuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika ambalo kwa sasa linafanyiwa ukarabati ili kuliongezea ubora na kuhifadhi historia yake alipotembelea Ofisi ya Mratibu wa Programu ya Ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam,(wa kwanza kushoto) Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika (katikati) akitoa maelezo ya utekelezaji wa Programu kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) alipotembelea Ofisi ya Programu hiyo leo Jijini Dar es Salaam, (wakwanza kulia)Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili.

…………………………………………………….

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi aagiza Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuhakikisha wanarasimisha Programu ya Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika.

Dkt.Possi ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Ofisi ya Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa Programu hiyo pamoja na kufahamu mpango wa kuiendesha.

“Kaeni pamoja na muandae Mpango Mkakati pamoja na Maandiko ya kuomba Ufadhili wa Programu na mpango huo uwe unatoa dira ya namna Programu itatekelezwa sababu niyakimataifa na siyo wa Tanzania pekee kwani kuna nchi za Afrika zinahusika na nchi za ulaya hivyo ni vyema kuwa na mpango madhubuti wa utekelezaji wa Programu hii,”alisema Dkt.Possi.

Akiendelea kuzungumza Dkt.Possi alisistiza kuwa kwanza Mratibu wa Programu anapaswa kuwa na Kanzi data ya Mawasiliano ya kila nchi iliyohusika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia katika ngazi za Kitaifa mpaka Kimataifa na hii itarahisisha utekelezaji wa shughuli za programu na usambazaji wa taarifa.

Pamoja na hayo nae Kaimu Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bw.Christopher Mhongole alieleza kuwa programu inamalengo makuu manne ambayo mojawapo ni Kuamsha Tafiti za Ukombozi wa Bara la Afrika,Kuenzi Mashujaa waliyopigania Uhuru pamoja na Kuratibu Programu kwa kushirikiana na nchi wanachama.

Aidha, Bw.Mhongole alieleza pia Programu hiyo ilianza kuratibiwa na Wizara kuanzia mwaka 2011 na shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wapigania uhuru wa kitaifa pamoja na ukusanyaji wa nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikizungumzia harakati ya ukombozi wa Bara la Afrika.

Halikadhalika nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili alikiri kupokea melekezo ya Kaimu Katibu Mkuu huyo na kueleza kuwa Idara itakwenda kuyafanyia kazi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rzLW8d
via

Post a Comment

0 Comments