Ticker

10/recent/ticker-posts

PROF. KABUDI AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifafanua jambo kwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi amemweleza Balozi Davutaglu kuwa Uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na mahusiano hayo ni imara hadi sasa. 
"Ushirikiano wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na ni imara kwa kweli, pamoja na mambo mengine uhusiano huu umekuwa ukijikita katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika shirika la ndege la Uturuki," Amesema Prof. Kabudi.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa, uhusiano wa Tanzania na Uturuki ni imara hivyo kwa sasa ni kuendelea kuimarisha uhusiano huo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali mfano kuwekeza katika sekta ya biashara na uwekezaji. “…naamini tukiwekeza katika viwanda hasa vya nguo hapa nchini ni fursa ambayo italiwezesha taifa la Tanzania kupata bidhaa nzuri na imara,". Amesema Prof. Kabudi

Kwa upande wake Balozi wa Uturiki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu amesema kuwa Uturuki ni nchi ambayo imekuwa ikiheshimu taratibu za nchi ya Tanzania na ni marafiki wazuri na wa siku nyingi hivyo ataendelea kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanasonga mbele ili kuiwezesha Tanzania kuwa na  maendeleo endelevu.

"Uwekezaji ni muhimu sana kwa nchi zetu hizi mbili na tayari nimeshawasiliana na Umoja wa Wasafirishaji na ule wa Mawakala wa Utalii Uturuki  ili waweze kutembelea Tanzania pamoja na kuangalia fursa za uwekezaji kwa lengo la kuwekeza na hatimaye kukuza sekta hizi na  uchumi wa mataifa haya mawili," Amesema Balozi Davutaglu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sh49I6
via

Post a Comment

0 Comments