POLISI NA RSA WAFANYA OPERESHENI YA KUSHTUKIZA

  Masama Blog      

Alanus Mbigi kutoka ofisi ya DTO Mombo akikagua Tairi kwenye moja ya bus la Abiria katika Eneo la Bwiko.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Solomon Mwangamilo akizungumza na Baadhi ya madereva katika eneo la Bwiko mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Muslimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin (aliyevaa miwani)Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga Eddo Mwakimwagile (wa kwanza kushoto)
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Muslimu,akizungumza na baadhi ya madereva wa Mabasi yanayotoka na kyingia Kanda ya Kaskazini ,mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro katika eneo la Bwiko.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin akizungumza katika kampeni abiria paza sauti eneo la Bwiko mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Tanga.
Mmoja wa Askari ofisi ya Taffic Korogwe Anna Mushi pamoja na Alanus Mbigi kutoka ofisi ya DTO Mombo akikagua Tairi kwenye moja ya bus la Abiria katika Eneo la Bwiko.
PC Hamis Mbilikila traffic kutoka ofisi ya Ofisi ya Rto Tanga akikagua tairi kwenye moja ya bus katika Eneo la Bwiko.
Mwenyekiti wa RSA mkia wa Tanga Eddo Mwakimwagile akitoa elimu kwa madereva wa mabus pamoja na wadau wa usafiri katika eneo la Bwiko
Mmoja wa Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji akitoa elimu kwa dereva namna ya kukagua kidhibiti moto mara unapotokea ndani bus na namna ya kuhakikisha mara zote wanakagua muda wa matumizi sahihi kwaajili ya usalama zaidi.
Mmoja wa Askari kutoka ofisi ya Traffic Korogwe Anna Mushi akiwa ndani ya bus akitoa elimu kwa Abiria juu ya usalama wao wawapo ndani ya chombo cha usafiri,aliyepo nae ni Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga.

Na.Vero Ignatus Tanga.

Jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama barabarani nchini kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani limefanya opereshani ya kushtukiza ya kufanya ukaguzi wa kwenye mabasi makubwa ya mikoani yanayotoka na kuingia kanda ya kaskazini mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro katika eneo la Bwiko

Operesheni hiyo iliyopewa jila la abiria paza sauti imeongozwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Fortunatus Muslimu kwa kushirikiana RSA, pamoja Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Tanga pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani mkoani hapa

Akizungumza katika operesheni hiyo Kamanda Muslimu amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi sana ya ajali za barabarani ,hivyo wamelazimika kuendesha operesheni hiyo ili kudhibiti wimbi la ajali hususani zinazotokea mwishoni na mwanzoni mwa mwaka

Amesema kwa kupitia kampeni hiyo ya abiria paza sauti amesema kutokana na kwamba jeshi la polisi barabrani ni wachache hivyo wameamua kushirikiana na RSA ili kuwafichua madereva wanaokiuka na kutofuata sheria na kanuni za usalama barabarani.

Amesema kuwa kampemni hiyo ni endelevu nchi nzima na imelenga kuhakikisha kwamba ajali za barabarani zinapungua na kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa madereva na makundi mengine amabao wanatumia barabara ili wanafuata sheria za usalama barabarani

''Maisha ya abiria hawa mnaowaona kwenye magari yanawategemea ninyi madereva na kipindi hilki cha mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka matumizi yavyombo yanakuwa mengi barabarani watu wanatoka sehemu mioja kwenda nyingine kufanya biashara,likizo kusalimua ndugu na marafiki wengine wanakwenda kwenye starehe,kwenye sikukuu za Christmass na mwaka mpya.Alisema Kamanda Muslimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin amewataka baadhi ya madereva kutokutem bea kwa mwendo kasi na kusingizia kwamba watu wamekuwa wakitoa kafara badala yake waweze kufuata sharia za usalama barabarani ili waweze kwa salama wao pamoja na Abiria

''Tukiwa huku barabarani tunatoa elimu msije mkawaona askari ni maadui yote haya tunakumbushana ili sharia za usalama barabrani zifuatwe

Amewaoma Madereva wote kufuata sharia za usalama barabarani na kuzingatia yale yote yanayopaswa kufuatwa ili kuepusha ajali za barabarabarani zinazopelekea vifo na ulemavu wa kudumu"


Amesema kuwa madereva wasipokuwa makini na kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za usalama barabarani kama inavyohitajika wanaweza kusababisha ajali, vifo,ulemavu wa kudumu na nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha usalama baraarani mkoa wa tanga Solomon amewataka madereva kuzingatia yale yote ambayo wamepewa elimu hiyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika kwa kuzingatia moja kwa moja kanuni na sharia za usalama barabarani ili kuwafikisha abiria salama katika safari zao

''Natumaini kuwa mtayazingatia haya mwanzo mwisho wa safari nanyi mtakuwa mabalozi wazuri kwa wenzenu na kuwaambia nini cha kufanya barabarani mbiyo hazikupi Maisha wala chochote unachokitafuta maishani Zaidi mbio zitakupa ulemavu ama kifo

Amewataka madereva kutokuwa chanzo cha matatizo bali waungane na wengine ili kuhakikisha kuwa barabara zote zinakuwa salama bila kusababisha ajali na kupoteza maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.

Kwa upande wao Wensley Olomi madereva wa Hai Express na amesema kuwa mpango huu wa kutokomeza ajali umesaidia kwa kiasi kikubwa kwani tangia mpango huo umeanza ajali zimepungua kwa kiasi kikubwa sana

‘’Tulikuwa tumezowea kila mwaka mwezi wa kumi na mbili tunasikia bus Fulani limeyua watu kadhaalakini siku hizi hakuna kitu kama hicho’’


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YQeXsH
via
logoblog

Thanks for reading POLISI NA RSA WAFANYA OPERESHENI YA KUSHTUKIZA

Previous
« Prev Post