Ticker

10/recent/ticker-posts

OPERESHENI YA KUKAMATA WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI WA NOTI BANDIA TANZANIA

***********************************
Benki Kuu ya Tanzania ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imeendesha operesheni ya kukamata watengenezaji na wasambazaji wa noti bandia nchini.
Operesheni hio iliyofanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro na Dar es Salaam, ilifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa  wawili ambapo mmoja wao ni wakala mkubwa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na mwingine ni mkazi wa Chanika ambaye ni mtengenezaji na msambazaji wa noti bandia jijini Dar es Salaam. 
Katika upekuzi uliofanywa na kikosi kazi kilichosimamiwa na jeshi la polisi, fedha bandia pamoja na mitambo mbalimbali na vifaa vyakutengenezea noti hizo vilipatikana ambavyo ni pamoja na 
  • Scanner
  • Vibao vyenye vichwa vya picha za marais mbalimbali walioko kwenye noti za kila nchi
  • Wino na rangi za aina mbalimbali zinatotumika kutengeneza noti bandia
  • Brush za kusafishia wino uliopakwa kwenye karatasi
  • Mashine ya kugandisha wino kwenye karatasi (lamination machine)
  • Desktop Computer aina ya dell na monitor aina ya HP ambayo hutumika kuchanganya rangi za noti kwakutumia software ya Adobe
  • Colored printer aina ya Xerox wanayotumia kuchapisha noti bandia
  • Mashine yakubana foil paper kwenye noti bandia ili kuipa mng’ao kama noti halisi
  • Mashine ya kukatia karatasi zenye picha ya noti ili ziwe katika sura 
Vielelezo vilivyokamatwa ni 
  • Noti za 10,540 Tanzania zenye thamani ya Tshs 11,748,000.00 (kama zingekua halali)
  • Noti 133, 048 za Marekani zenye thamani ya dola 13,302,400 (kama zingekua halali)
  • Noti 11,0233 za Mozambique zenye thamani ya Tshs 290,464,259.98 (kama zingekua halali)
  • Noti 2270 za Kwacha ya Demokrasia ya Kongo zenye thamani ya KWACHA 4,302,000 (kama zingekua halali)
  • Noti 1 ya shilingi ya Kenya yenye thamani ya Kshs 200
  • Noti 1 ya Kwacha 500 za Malawi
Karatasi 65 zenye picha za pesa za nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zambia, Dola za Marekani, DRC Congo, Tanzania, Botswana na Mozambique


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PD2iGA
via

Post a Comment

0 Comments