Ticker

10/recent/ticker-posts

NHIF Yawapiga Msasa Wanahabari Mkoa wa Mbeya Kuhusu Vifurushi vya Bima ya Afya


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Bernard Konga akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kutumia vyombo vyao vya habari kuwaeleza wananchi faida za kujiunga na vifurushi vipya kwani vimezingatia makundi yote katika jamii kwa lengo la kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa huduma ya matibabu. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF)Bw. Christopher Mapunda akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo alisema kuwa viwango katikavifurushi vya bima ya afya sio gharama za matibabu bali ni uchangiaji ndio maana hata ukiumwa na kutumia zaidi ya kiwango cha laki moja na tisini na mbili, mfuko utagharamikia matitabu hayo. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Hipoliti Lello na akitoa mada kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwaeleza kuwa mpango wavifurushi sio mpya na NHIF imeanzisha mpango huo kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi kulingana na mahitaji yao. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya.
wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakifuatilia uwasilishaji wa mada kutoka kwa wataalam wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF), Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

**************************
NA MWANDISHI WETU, MBEYA

Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Umewapiga Msasa wanahabari Mkoa wa Mbeya kuhusu Vifurushi vya Bima ya Afya na kuwasisitiza kutumia kalamu zao kuwaeleza wananchi umuhimu wa kujiunga ili kuwa na uhakika wa matibabu. 

Akiongea wakati wa Kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amewaeleza wanahabari hao kuwa kwa namna ambavyo mfuko umetengeneza vifurushi umezingatia gharama za matibabu ya kawaida ambayo ukienda hospitalini lazima uyapate. 

“Leo hii wapo wanaopotosha kuhusu gharama hizi, hatuwezi kuwaacha watanzania ambao wapo tayari kutumia bima ya afya ili kupata matibabu na kusema tusubiri, niwahakikishie tumefanya tafiti, kiasi cha Shilingi laki moja na tisini na mbili kimezingatia gharama za matibabu ya kawaida ambayo ukienda hospitalini lazima uyapate na utaratibu huu ni niwa hiari”-Alisema Bw. Konga. 

Aidha, Bw. Konga alisema kuwa umefika wakati kwa wananchi kujikatia bima ya afya kabla ya kuugua hasa katika kipindi hiki ambacho mfuko umeanzisha mpango wa vifurushi ili kuwa na uhakika wa matibabu na kupuuza maneno ya baadhi ya watu wanaoendesha mijadala isiyo na tija. 

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko huo Bw Christopher Mapunda alisema kuwa viwango katika vifurushi vya bima ya afya sio gharama za matibabu bali ni uchangiaji tu na ndio maana hata ukiumwa na kutumia zaidi ya kiwango cha laki moja na tisini na mbili, mfuko utagharamikia matitabu hayo bila kujali kuwa umetibiwa kwa kiasi gani. 

Awali akiongea wakati akiwasilisha mada kwa wanahabari hao Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Hipoliti Lello alisema kuwa mpango wa vifurushi sio mpya na NHIF imeanzisha mpango huo kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi kulingana na mahitaji yao


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2LZzWDV
via

Post a Comment

0 Comments