Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KANYASU ALIPONGEZA TAMASHA LA ‘ LAMADI UTALII FESTIVAL’

 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera akizungumza katika tamasha hilo
 Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Bi. Diana Chambi akizungumza kwenye uzinduzi huo

NA ANDREW CHALE, BUSEGA

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameiomba Wilaya ya Busega kuweka ratiba ya tamasha la Lamadi Utalii Festival kufuatana na msimu [season] wa utalii nchini ili kuunganisha watalii wanaotembelea Hifadhi ya Serengeti wawezea kutembelea na tamasha hilo.

Kanyasu ameyasema hayo jana wakati akizindua tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni msimu wake wa kwanza kufanyika.

"Nawapongeza Wilaya ya Busega kwa kuandaa tamasha ili la Utalii. Nakupongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Busega.

Kupitia tamasha ili lazima tutangaze vuvutio tulivyo navyo. Lakini pia nawaomba kwamba kuweka ratiba kufuatana na msimu‘season’ za utalii nchini ili tuunganishe watalii wetu na matamasha haya wanapokuja waweze kutoka Serengeti waweze kuja kutazama ngoma zinazoendele hapa.

Lakini tupanue mialiko tuwe na vikundi vingi zaidi vya ngoma kutoka maeneo mbalimbali kama wanavyofanya maeneo mengine kwa hiyo naamini tukiyakuza kwa ‘style’ hiyo yatakuwa na mtazamo mpana na watu watapenda kuja kutazama’ alieleza Naibu Waziri Constatine Kanyasu.

Aidha, Kanyasu amewataka Wananchi wa Lamadi Busega kuhakikisha wanalinda wanyama pamoja na kulinda wawekezaji.

"Ni jukumu letu kuwalinda Wanyama. Pia wenyeji muwalinde wageni watalii tunaamini mtapata wawekezaaji wengi alisema Kanyasu.

Katika kuhakikisha tamasha hilo linafikia hadhi ya juu kama matamasha mengine, Kanyasu ameeleza kuwa, kwa sasa Serikali imeamua kuondoa ‘single entry’ ambapo kwa sasa Mtalii anaweza kutembelea Hifadhi ya Serengeti na mtalii huyo huyo akatembelea Lamadi na kuweza kujionea tamasha hilo na maeneo mengine yenye vivuti ndani ya Wilaya Busega.

"Awali suala la ‘single entry’ lilikua likiua utalii wa maeneo mengi hivyo Bunge limeamua kuondoa hiyo na sasa mgeni anapata nafasi ya kuingia kokote kwani anaweza kushuka KIA na anaweza kwenda Serengeti na kisha akaingia Lamadi kutazama vivutio vya utalii vya hapa pamoja na maeneo yenye utamaduni ikiwemo kabila la wasukuma na ngoma zao" alisema Kanyasu.

Katika hatua nyingine, Kanyasu amesema Wizaya yake inatarajia kuja na boti kubwa mpya ambayo itakuwa ni ya kisasa na itatembeza watalii kwenye Zictoria.

"Tunatengeneza boti mpya hii itakuja hapa na kwenda hadi Burigi Chato na maeneo mengine ya vivutio ndani ya Ziwa Victoria.

Maeneo ya ziwa letu lina fukwe na mwaro mzuri zenye vivutio hivyo tunataka kuzitumia kwa sasa" alisema Kanyasu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati wa Tamasha hilo na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera alipongeza wananchi na wadau kulipokea tamasha hilo kwani wao ndio chachu ya katika kufanikishwa kwake.

"Lamadi Utalii Festival tumelianzisha lengo ni kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya Utalii, lakini pia kuhamasisha wananchi kufanya Utalii wa ndani ili wawe mabalozi wa kutangaza vivutio vyetu tulivyonavy" alieleza Mkuu wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera.

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Bi. Diana Chambi alisema tayari wameanza kutoa elimu ya awali ikiwemo ya kudhibiti wanyama pamoja na ku kuunda vikundi na kuviwezesha.

"Tupo pamoja wananchi wa Busega muda wote na tayari tumenza kutoa elimu mbalimbali ya namna ya kudhibiti tembo kama njia mbadala ikiwemo ya kutumia pilipili na pia tunashirikiana na wananchi kwa kuunda vikundi ambavyo tunaviwezesha ili waweze kuwa mstari wa mbele wa kuweza kutoa huduma ya kwanza kwa wanyama wanaovamia maeneo kabla sisi hatujafika.

Kwa hiyo bado tunambinu zingine mbalimbali ilikufundisha vikundi na kufikia maeneo yote yanakuwa salama" alisema Diana Chambi.

Katika tukio hilo wageni mbalimbali wameweza kufika wakiwemo viongozi wa dini, kimira, wakuu wa taasisi, wafanyabiashara, wajasiriamali sambamba na Mbunge wa jimbo la Busega, Dkk. Rafael Chegeni.

Katika siku ya kilele cha tamasha hilo, Januari Mosi, 2020 kutakuwa na tukio la kwenda hifadhi ya Serengeti na gharama ni Tsh. 55000, kwa kila Mtanzania lakini watoto 10 wa mwanzo wao watalipiwa Tsh. 50,000 pekee kama ofa. Gharama hiyo itajumlisha usafiri wa kutoka na kurudi Lamadi, ada ya kiingilio, chakula cha mchana, vinywaji laini.

Mgeni rasmi pia alipata kutembelea mabanda ya maonesho pamoja na kujumuika pamoja ikiwemo kucheza ngoma za asili katima tamasha hilo.

Tamasha hilo kwa mwaka huu ni la kwanza na kudhaminiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wadau wengine mbalimbali huku likiwa na Kauli mbiu ya "Utalii wa Ndani Unawezekana".


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36dcYBl
via

Post a Comment

0 Comments