Mwakyembe aipongeza Kili Marathon kwa kukuza utalii wa michezo

  Masama Blog      
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa kukuza utalii wa michezo kwa kupitia mbio hizo na kuwataka waandaaji wengine nchini kuiga mfano huo.

Alitoa pongezi hizo wakati wa Kikao maalumu na waandaaji hao wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon kufuatia uzinduzi wa kufana uliofanyika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe ndiye alikuw amgeni rasmi na baada ya hapo aliamua kuwaalia waandaaji hao ofisini kwake ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza riadha nchini.

Kamati ya maandalizi ya Kilimanjaro Marathon iliwakilishwa na Muandaaji Mkuu John Addison ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wild Frontiers na pia aliyebuni wazo la Kilimanjaro Marathon, Aggrey Marealle ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Executive Solutions kampuni inayoratibu mbio hizo kitaifa na John Bayo ambaye ni mkurugenzi wa mbio hizo kitafa. Wote hawa ni waanzilishi wa mbio hizo zilizoanza 2003.

Kwa kuzingatia kuwa Kilimanjaro Marathon ina washiriki zaidi ya 11,000 kutoka nchi 58 duniani, Waziri Mwakyembe alisema kuna haja ya kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya Wizara yake na ile ya Maliasili na Utalii ili kukuza maendeleo ya michezo na utalii.

“Kilimanjaro Marathon imekuza utalii wa michezo kwa kiasi kikubwa kwani washiriki wanaweza kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii katika mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine nchini ambapo kuna vivutio vya utalii,” alisema na kuongeza kuwa riadha ni nzuri kwa afya lakini pia ni moja ya chanzo cha fedha za kigeni kwa Tanzania.

Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa miko ayote inayoandaa mbio mbalimbali kuhakikisha wanazingatia faida yam bio hizo kiuchumi kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kitamaduni na kijamii kwa wenyeji na watalii kabla na baada yam bio  ili kuongeza kipato na ajira kutokana na shughuli hizo za wiki nzima.

Alionesha pia kufurahishwa na namna mbio mbalimbali zinaanzishwa mikoani ila akatoa tahadhari kuwa ni muhimu kuwepo na miongozo na vigezo  kuzingatiwa huku akimtaka Mkurugenzi wa Michezo kuhakikisha hili linasimamiwa vikamilifu.

Wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2020 ni Kilimanjaro Premium Lager-42 km, Tigo-21 Km, Grand Malt-5km. Wengine ni  Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Barclays Bank na watoa huduma maalumu ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.                            

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe ametoa pongezi nyingine kwa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon kwa kukubali kusaidia kufanyika kwa Mbio za John Steven Akhwari ambazo zinatarajiwa kufanyika Juni mwakani.

Waandaaji hao wanafanya kazi na wadau wengine wakiwemo Chama Cha Riadha Tanzania na Taasisi ya John Steven Akhwari ili kuweka vigezo mbalimbali  na kuhakikisha mbio hizi zinafanikiwa ili kumtambua Bw. Akhwari ambaye anatambulika na  Olympiki kama mwanarisha anayewakilisha dhamira ya Olympiki.

Akizungumza kwa niaba ya waandaaji, Bw. Marealle alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuunga mkono mbio hizo miaka yote  jambo ambalo limewapa waandaaji na wadhamini heshima ya kipekee. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Harison Mwakyembe (katikati) na Mkurugenzi wa Michezo Yussuf Singo (kushoto) wakiwa na waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager baada ya Kikao cha pamoja kilichoitishwa na Waziri ili kujadili namna ya kuendeleza riadha nchini. Wengine kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Executive Solutions ambao ndio waratibu wa mbio hizo kitaifa, Aggrey Marealle, Muandaaji Mkuu wa mbio hizo ambaye pia ni Afrisa Mtendaji Mkuu wa Wild Frontiers, John Addison na Mkurugenzi wa Mbio hizo Kitaifa, John Bayo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2E31wMt
via
logoblog

Thanks for reading Mwakyembe aipongeza Kili Marathon kwa kukuza utalii wa michezo

Previous
« Prev Post