Ticker

10/recent/ticker-posts

MWAKILISHI JIMBO LA CHUMBUNI AITAKA UWT KUSHIRIKIANA KUKIIMARISHA CHAMA

Na Mwashungi Tahir Maelezo.

Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwanza amewataka akinamama wa Umoja wa Wanawake UWT wa Wilaya ya Amani kuweka mashirikiano katika kukimarisha chama ili kiweze kukipatia ushindi ifikapo 2020.

Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Tawi la CCM Kilimani wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la UWT Wilaya ya Amani na kuwataka kuzidisha mashirikiano kwa lengo la kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Amesema hivi sasa wakati wa Daftari la kudumu umeshafika hivyo akinamama wasimame katika kuhamasisha kwenda kujiorodhesha na pia kuwahimiza vijana waliofikia umri wa miaka kumi na nane kwenda kujiandikisha ili waweze kupiga kura.

Aidha alisema Daftari linahitaji kuimarishwa kuhamasishwa na kutiwa hamasa ambapo akina mama wa UWT ndio Viongozi wasimamizi wa mambo mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kushajihisha wanachama kwenda kujiandikisha kwa wingi bila ya kufanya ajizi.

"Daftari limeshafika tuitumie fursa kwa ujiandikisha kwa kila mwenye sifa na vijana wetu tuwahimize kwa kila alofikia umri", alisema mwakilishim huyo.

Pia alisema ndani nya Nchi yetu ili tuweze kupata maendeleo zaidi na amani na utulivu iweze kudumu ni lazima tuhakikishe chama kinapata ushindi wa kishindo kwani historia ya nchi yetu ni kuidumisha amani iliyopo ambayo ni hazina kubwa kwa chama na wananchi wake .

Hivyo amewataka akinamama kukaa na kuweza kujitathmini kwa kujua wapi walipotoka na wanakokwenda na kuweza kuona jinsi nchi ilivyoweza kupiga hatua na kupata mafanikio makubwa kwa kusimamia chama cha Mapinduzi.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Amani Fatma Hamrani amewataka akina mama kuliongoza gurudumu la maendeleo hadi kulifikisha ukingoni kwa salama na kupiga kura kwa amani na kudumisha mashirikiyano yaliyokuwepo.

Nae Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Asha Mzee Omar akisoma taarifa ya utendaji wa kazi za UWT kwa Kipindi cha January hadi Decemba 2019 alisema uhai wa chama ndani ya Wilaya hiyo imezidi kuimarika zaidi kwa kuongeza wanachama wapya 1,454 ambapo zamani walikuwa 3,573 na kuweza kufikia 5,027.

Alisema kwa upande wa siasa ndani ya wilaya ya Amani ni nzuri wanachama na wananchi wanaendelea kufanya kazi na mambo mengine ya kujitafutia maisha bila bughudha .

Pia alisema wanachama na wananchi wa Wilaya ya Amani wanampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein kwa kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi , miundo mbinu , huduma za kijamii , Amani na Utulivu katika uongozi wake wa miaka tisa ndani ya Zanzibar.

Mada mbili ziliwasilishwa katika Baraza hilo ikiwemo Umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi na Uandaaji wa Taarifa za kazi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37mh3Ua
via

Post a Comment

0 Comments