MUUGUZI ANAYETUHUMIWA KUBAKA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI.

  Masama Blog      
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- Katavi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani Katavi

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

"Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika  ".Amesema Waziri Ummy

Aidha,amewataka watumishi  wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao

“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili,weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za nidhamu ikowemo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya dola"Amesisitiza Waziri Ummy.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Z9ZzY1
via
logoblog

Thanks for reading MUUGUZI ANAYETUHUMIWA KUBAKA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI.

Previous
« Prev Post