Ticker

10/recent/ticker-posts

MTAKA TAIFA CUP 2019 KUFANYIKA SIMIYU DESEMBA 27-31

NA ANDREW CHALE

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linatarajia kuwa na Mashindano ya kombe la Taifa la Kikapu (Mtaka Taifa Cup 2019) yatafanyika mkoani Simiyu tarehe 27 hadi 31 Dec 2019 sambamba na mkutano mkuu wa mwaka.

Kwa mujibu wa Rais wa TBF, Phares Magesa amesema kuwa Mashindano haya yatashirikisha timu za mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani za wanawake na wanaume.

Aidha, mbali na michuano hiyo, TBF inatarajiwa kufanya Mkutano wake  Mkuu Desemba 29, pamoja na mambo mengine huku pia kukitarajiwa kuwa na semina kwa viongozi wote wa vyama vya mikoa na Taifa kuhusu Uongozi, utawala na masoko.

"Desemba 29 TBF tutafanya mkutano mkuu. Pia kikao hicho kitajadili na kupitisha  mpango kazi wa TBF na kufanya maboresho /mabadiliko ya katiba ya TBF na mengineyo" alieleza Magesa.

Rais huyo wa TBF aliipongeza timu ya Kikapu ya JKT ambayo imetuwakilisha katika mashindano ya kufuzu kucheza ligi ya Kikapu Afrika 'Basketball Africa League (BAL)' yaliyofanyika Kigali Arena, Rwanda 17-22 mwaka huu.

Mashindano haya ya kufuzu BAL yalishirikisha timu 16 tu ambazo ni mabingwa wa ligi za nchi zao kutoka nchi 16 na ambao wamefuzu kutoka katika BAL mzunguko wa kwanza na kufanikiwa kucheza mashindano haya ya BAL  'Elite 16' (ambapo timu 8 zilichezea Kigali, Rwanda kanda ya mashariki na timu 8 zilichezea  Yaounde, Cameron Kanda ya magharibi).

" JKT kufika hatua hii ni mafanikio makubwa katika historia ya kikapu Tanzania yaani kuwa miongoni mwa vilabu 16 bora Afrika nzima.

Pongezi nyingi sanqa kwa kijana wetu Mtanzania Baraka Sadik Athumani kwa kuwa mfungaji bora wa mashindano ya FIBA Zone V na BAL mzunguko wa kwanza kwa Afrika nzima, ameiletea sifa nyingi nchi yetu na mafanikio makubwa kwa Tanzania" alisema Magesa.

Na kuongeza kuwa: TBF inawapongeza sana timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzania ya wasichana wa U16 ambao nao mwaka huu wametuwakilisha katika mashindano ya kombe la Kikapu la Afrika (U16 Afrobasket 2019) ambayo nayo ilifanyika Kigali.

"Pamoja na matukio mengi ya Kitaifa na Kimataifa, matukio mbalimbali yaliyo mbele yetu ni : Mashindano ya kutafuta nafasi ya kufuzu Kombe la Afrika (Afrobasket Preliminaries) yanafanyika  14-18 Januari, 2020 Nairobi, Kenya.

Timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzania Wanaume itatuwakilisha." Alieleza Magesa.

Megesa pia alisema kuwa, April 2020 tunatarajia kuwa wenyeji wa FIBA Africa Zone V U18 Boys and Girls Nations Championship, Dar es Salaam, Tanzania.

"Tunaomba wadau na wafadhili mjitokeze kushirikisha nasi kusaidia kufanikisha ushiriki wetu katika matukio haya ya kimataifa na kitaifa.

Kutokana na uwingiliano wa  matukio mengi tunaomba mikoa iwasilishe haraka iwezekanavyo ratiba zao za mwaka mzima na mipango kazi yao ili TBF iweze kutoa Kalenda ya TBF mwaka 2020 na kuiwasilisha katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT)" alimalizia Magesa.

TBF imekuwa mstari wa mbele katima kuinua michezo ya mpira wa kikapu hapa nchini ambapo pia imekuwa chachu ya wacheza mbalimbali nyota kutoka mataifa mengine ikiwemo Marekani kuja kusaka vipaji na kuendeleza kliniki ya michezo hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QeGlwl
via

Post a Comment

0 Comments