Ticker

10/recent/ticker-posts

Mradi wa REGROW kuanza kumaliza changamoto za miundo mbinu hifadhi ya Taifa ya Ruaha Inbox x

Na Francis Godwin ,Iringa


KATIBU mkuu wizara ya maliasilia na utalii Prof Adolf Mkenda amesema wizara yake imejipanga kupitia mradi wa kuendeleza Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania(REGROW) kuboresha miundo mbinu ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa ili kuweza kuvutia idadi kubwa ya watalii zaidi .

Akizungumza jana baada ya kuzindua vitendea kazi vya mradi wa REGROW katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha katibu mkuu huyo alisema kuwa wizara hiyo imeelekeza nguvu zake kutangaza na kuboresha miundo mbinu katika hifadhi ya Ruaha ili kuiwezesha hifadhi hiyo na hifadhi nyingine kuendelea kujiendesha kwa faida na kutoa gawio lake serikalini .

Kwani alisema changamoto ya miundo mbinu katika maeneo ya hifadhi mbali mbali hapa nchini imekuwa kikwazo kikubwa kwa watalii kufika kutembelea hifadhi nchini na kama miundo mbinu itaboreshwa watalii zaidi wanaweza kufika kwa urahisi zaidi .

Alisema changamoto kubwa ya hifadhi ya Ruaha ni pamoja na ubovu wa miundom mbinu na kuwa kupitia mradi wa REGROW wizara imejipanga kuanza kuboresha miundo mbinu hiyo na kutangaza hifadhi ya Ruaha ili kuwezesha kuongeza kasi ya watalii kufika .

Prof Mkenda alisema changamoto ya utalii ina vitu viwili vikubwa kwanza kufungua miundo mbinu ndani ya hifadhi yenyewe na namna ya kufikia ndani ya hifadhi hivyo mradi huo unasaidia mambo makubwa mawili kutangaza na kuboresha miundo mbinu yake .

Alisema ndani ya hifadhi ya Ruaha wanategemea kupitia mradi huo wa REGROW kufungua barabara ya kuunganisha mkoa wa Mbeya na Dodoma kwa kujenga daraja kubwa katika eneo la Othuman ambalo kuna mzungu alipata kujenga daraja kabla ya hifadhi hiyo kutangazwa rasmi kuwa kujengwa kwa daraja eneo hilo kutawezesha kuunganisha hifadhi hiyo na watalii wakaweza kuingia kutokea Dodoma na kutokea Mbeya kwenda hifadhi nyingine kama Katavi na Kitulo .

Hata hivyo alisema wakati wizara inaendelea kufanya jitihada za kutangaza utalii na kuboresha miundo mbinu mbali mbali kwenye hifadhi nchini bado itatoa wito kwa wadu wa utalii nchini kuunga mkono jitihada za kutangaza utalii kwa kutenga gharama zao wenyewe badala ya kusubiri kuwezeshwa na wizara ya maliasi na utalii kwa kila jambo wanalotaka kufanya .

Kwani alisema wapo baadhi ya wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi ambao wameendelea kutangaza utalii nchini kwa kutumia gharama zao wenyewe .

Japo alisema wizara itaendelea kuwatumia watu wa makundi mbali mbali watu maarufu kwa ajili ya kutangaza utalii nchini japo watafanya hivyo kwa kushirikisha idara mbali mbali zinazohusiana na makundi hayo ili kuweka vigezo vya kuwapata wale watakaofanya kazi ya kutangaza utalii na mwisho wa siku kuja na matokeo ya kazi hiyo .

Prof Mkenda alisema kuwa wakati wanaendelea na uboreshaji wa miundi mbinu katika hifadhi nchini bado wizara inaangalia jinsi ya kuanzisha utalii wa meli na fukwe ili kuvutia watalii zaidi nchini kwani wapo baadhi ya watalii ambao wanatamani kuja kutalii katika hifadhi za fukwe na utalii wa meli na kuwa jitihada zitakazofanyika ni kujenga magati kwa ajili ya utalii wa meli na kuboresha maeneo ya fukwe .

Kamishna mwandamizi wa uhifadhi wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) kanda ya kusini Dk Christopher Timbuka alisema kuwa ujio wa mradi wa REGROW umetokana na changamoto ambazo hifadhi za kusini zilikuwa zikikabiliwa nazo .

Kuwa changamoto hizo ni miundo mbinu kuwa mibovu na watalii kushindwa kufika katika hifadhi hivyo mradi huo utawezesha kufungua utalii nyanda za kusini .Hivyo alisema ujio wa mradi huo ambao unaanza kazi utasaidia kuongeza idadi ya watalii na kuongeza idadi ya vitanda kutoka vitanda 400 vilivyopo na kuongezeka zaidi ili watalii kuweza kupata maeneo ya kufikia .

Alisema kupitia mradi huo ulinzi ulinzi didhi ya ujangili kwenye hifadhi utapungua zaidi kutokana na mradi huo kuwezesha vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi .

Mratibu wa mradi wa REGROW Saanya Aenea alisema kuwa vifaa mbali mbali vimezinduliwa kwa ajili ya mradi huo na kuwa changamoto kwa asilimia 100 zitakwenda kumalizika .

Pia alisema kwa kupitia mradi huo wananchi watajengewa miradi ya kiuchumi kama ya ufugaji samaki ,ufugaji nyuki na mingine ili kuwawezesha kiuchumi na wasiwe chanzo cha kujihusisha na ujangili .
 Kamishina mwandamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) kanda ya nyanda za juu kusini Dkt Christopher Timbuka wa pili kulia akimkabidhi baadhi ya vifaa vya mradi wa Regrow, katibu  mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda ,mradi wa Regrow umekabidhi vifaa vya ulinzi hifadhi ya Ruaha vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.2
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/387QiE4
via

Post a Comment

0 Comments