MKUU WA WILAYA NYASA ASEMA WANANCHI WANASUBIRI KWA HAMU KUBWA UJIO MELI MPYA YA ABIRIA NA MIZIGO

  Masama Blog      
 Meli ya MV.Mbeya II ikiwa imeegeshwa baada ya ujenzi wake kukamilika ambapo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema wananchi wa wilaya yake wanaisubiri kwa hamu meli hiyo ambayo inakwenda kuonda changamoto ya usafiri kayika Wilaya ya Nyasa.
 Moja ya jengo la bandari ya Mbambabay ambayo tayari TPA imeweka mkakati wa kuiboresha kwa kujenga bandari kubwa ambapo kwa sasa tayari wameshaweka mkakati wake.


 Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Isabela Chilumba akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa TPA kuboresha miundombinu ya usafiri wa meli katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Abedi Gallus akizungumza kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kujenga miundombinu ya bandari katika ziwa hilo.

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Nyasa

MKUU wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Isabela Chilumba amesema kazi ya ujenzi wa miundombinu ya bandari katika wilaya hiyo na kukamilika kwa meli tatu ndani ya Ziwa Nyasa kunakwenda fungua fursa ya kiuchumi na wananchi wanasubiri kwa hamu ujio wa meli hizo kwenye eneo lao.

Hivyo amesema wanaishukuru Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kwa hatua iliyochukua ya kuanza kuboresha huduma ya usafiri ndani ya Wilaya ya Nyasa kwa kutumia usafiri wa bandari na hamu ya wananchi ni kuanza kwa safari ya meli mpya ya Mbeya II.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu huyo wa Wilaya ya Nyasa ametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina umuhimu wa kuboreshwa kwa miundombinu ya usafiri wa majini hasa kwa kuzingatia wao wanautegemea zaidi.

"Hapa kwetu Nyasa tuna bandari ya Mbamba Bay na Tumbi, na tunaishukuru TPA kwa kuweka mkakati wa kuboresha bandari hizi ambazo kwetu ni muhimu sana kwa shughuli mbalimbali za kijami ikiwemo ya kusafirisha abiria na mizigo.Wananchi wetu wanatumia zaidi usafiri wa majini a kukosekana kwa usafiri huo meli au vyombo vya usafiri ni changamoto.

"Watu wanalazimika kutumia maboti au mitumbwi kwa safari za mbali na wengine wanakwenda hadi Msumbuji a Malawi kwa usafiri huo lakini kwa safari za kwenda Kyela kupitia Ludewa ni changamoto.Kwa sasa hivi tunasubiri meli mpya ambayo tumeahidiwa ya abiria.

"Na tunategemea Januari mwaka 2020 inaweza kuanza kufanya kazi na kwa maendeleo ya wananchi wa Nyasa itakuwa fursa kubwa kwa wao kuweza kusafiri kwa urahisi kwa kutumia usafiri wa maji.Kama mnavyofahamu safari za majini kwenye meli gharama zake ni za chini kuliko barabara,"amesema.

Hata hivyo amesema tayari kuna meli mbili za mizigo ambazo zimeanza kufanya kazi ambazo ni MV.Ruvuma na MV.Njombe ambazo hizo ili zifanye kazi kwa ufanisi zinategemeana na barabara , hivyo wanaishukuru Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kuwajengea barabara yao kwa kiwango cha lami kutoka Mbinga hadi Mbambabay yenye urefu wa kilometa 67 na sasa tayari kilometa 32 zimekamilika kwa kiwango cha lami.

"Kwa mujibu wa matarajio na ahadi ya mkandarasi ifikapo Septemba mwaka 2020 atakuwa amekamilisha, kwa hivyo kukamilika kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ndio itakuwa fursa kwa meli za mizigo kufanya kazi muda wote kwani ubovu wa barabara na uwepo wa kona nyingi ulisababisha magari makubwa ya mizigo kushindwa kupita lakini sasa barabara inajengwa, magari mengi ya mizigo yatakuja kwenye katika bandari zetu.

"Tuaamini wataoakuwa wanapeleka mizigo yao mkoani Mbeya watapitisha katika bandari zetu, hivyo unaiona Nyasa ijayo itakavyokuwa kiuchumi.Pia wapo wanaosafiri kutoka Kyela, Mbinga na maeneo mengine ya Nyasa mpaka Mbambabay ambao hao nao watatumia bandari zetu,"amesisitiza.

Ameongeza katika Wilaya ya Nyasa kuna uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe yameanza kuchimbwa katika kijiji cha Malini ambayo ni makaa yake ni bora kuwahi kutokea kuchimbwa katika Mkoa wa Ruvuma, hivyo makaa hayo yatasafirishwa kwa usafiri wa meli.

"Hivyo tunaanza kuona fursa za kiuchumi, uwekezaji mkubwa wa shughuli mbalimbali na kuona ule uwekezaji wa viwanda unakwenda kutokea, ukiona sehemu kuna makaa ya mawe ambayo ni nishati muhimu katika shughuli za viwandani maana yake tunakwenda kufungua milango ya shughuli za viwandani.Meli tatu ambazo zitakuwa ndani ya Wilaya ya Nyasa nazo zinakuwa chachu ya maendeleo yetu na nchi kwa ujumla,"amesema.

Amesema kutokana na jitihada hizo za TPA na Serikali ya Awamu ya Tano, wananchi wako tayari na wanasubiri kwa hamu kuanza kutumia usafiri huo kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla kwani kwao usafiri wa majini ni fursa tosha kiuchumi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QsE9kY
via
logoblog

Thanks for reading MKUU WA WILAYA NYASA ASEMA WANANCHI WANASUBIRI KWA HAMU KUBWA UJIO MELI MPYA YA ABIRIA NA MIZIGO

Previous
« Prev Post