Ticker

10/recent/ticker-posts

MFK AUTOMOBILE YAZINDUA MAGARI YA KISASA AINA YA HONGYAN

 Wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa magari ya kisasa ya mizigo aina ya Hongyan wakishuhudia moja kati ya magari hayo, kampuni ya MFK Automobile Tanzania kushirikiana na Hongyan kutoka China walizindua magari hayo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa MFK Automobile Tanzania, Mehboob Karmali (kushoto) akikabidhiwa funguo na Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong kuashiria uzinduzi wa magari ya mizigo ya kisasa aina ya Hongyan yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki kwenye  hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Picha ya pamoja kati ya  Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula (wa nne kulia) na viongozi wa MFK Automobile Tanzania na SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China kwenye hafla ya uzinduzi wa Hongyan.


 Kampuni ya MFK Automobile ambayo inajihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari ya mizigo nchini, imezindua magari ya kisasa yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali alisema shukrani za pekee kwenu kwa kuitikia wito wetu wa mualiko wa uzinduzi wa vifaa vipya vya kampuni ya MFK, Gari ambazo kwa mara ya kwanza kuingia Afrika Mashariki aina ya HONGYAN. 

MFK ni kampuni mpya ambayo inajishughulisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari mbalimbali aina ya Tiper na Tracto head, tumekuja kuunga jitihada za serikali za kuelekea uchumi wa viwanda ambapo utawezesha fursa mbalimbali katika kukuza uchumi, tutatengeneza fursa kwa wasafiri na wasafirishaji na ndio sababu kuu iliyotufanya kuleta magari yenye teknolojia ya ulaya na umadhubuti wa China alisema Karmali 

Katika magari haya ya Hongyan, MFK Automobile inawapa Watanzania bidhaa yenye ubora kwa mtumiaji na mmiliki,bila usumbufu wowote na kiufundi wa gari hizi za HONGYAN, zina manufaa mengi kwa mmiliki kwa kumuwezesha kuhimili barabara zozote nchini, matumizi madogo ya mafuta na zina chumba cha kupumzika kwa dereva aliendelea kusema Karmali. 

Pia tumeona fursa katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo tumejipanga katika kuleta vifaa vyenye ubora ambavyo vitahakikisha Tanzania inakuwa kituo kikuu katika sekta hii kwenye ukanda huu wa Afrika ya mashariki na kati. 

“Lengo kuu la kampuni yetu ni kufanya Tanzania ipate bidhaa zenye ubora na za bei nafuu zinazoendana na kasi ya uchumi wa viwanda ambayo ni moja ya sera ya serikali ya awamu ya tano ili kufikia uchumi huo wa kati ifikapo mwaka 2025, MFK tunasimamia hilo”, alimalizia kusema Karmali. 

Tunajisikia fahari kufanya kazi na kampuni hii ya utengenezaji wa magari,katika ushirikiano huu wa IVECO GROUP NA WASHIRIKA WAO WA CHINA HONGYAN. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula alisema “sekta ya usafirishaji imetoka mbali sana nakumbuka tulianza tukiwa na malori aina ya Scania 682 hadi kufikia sasa tunatumia magari ya kisasa zaidi, tunawashukuru MFK kwa mpango huu wa kuleta magari haya ya kisasa, pia yatatufanya sisi wafanya biashara kuyanunua kwa umoja wetu tuuweze kufanya sekta hii ya usafirisahji kuwa pana zaidi ukanda huu,. Pia nawaomba mabenki yaweze kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa sekta hii kwani haina ubabaishaji kurudisha mikopo hiyo. alisema Ngalula. 

Aliongezea kusema Ngalula “tuna bidhaa nyingi sana zinahitaji usafirishaji kama vile mazao, shaba, madini mbalimbali, hii itasaidia kuweka vituo vya kufanyia huduma(service) za magari na kuuza vipuri mikoani ili kuepusha wizi unaotokana na madereva wasio waaminifu”. 

Hata standard gauge SGR itahitaji zaidi kushirikiana na sekta hii ya usafirishaji ili kuwafikishia mizigo kwa urahisi zaidi, huwezi kuwa na Treni bila kuwa na magari ya mizigo, ukizingatia usafirishaji wa kutumia barabara unahitajika kwa asilimia 75 . alimalizia kusema Ngalula. 

Nae Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, -MS Winnie Xiong alisema hii ni fursa ya kipekee kwa kampuni yetu kuleta magari haya nchini Tanzania, hasa ukizingatia Tanzania na china zimeweka mahusiano ya kidiplomasia miaka 55 hadi sasa tokea mwezi Aprili 26, 1964, nchi hizi mbili zimejenga uhusiano imara na kushirikiana bega kwa bega. Leo nawaahidi kuwa Hongyan itazalisha magari bora ya mizigo kwa soko la Tanzania kwa kupitia washirika wetu MFK na kuwawezesha wateja wetu kugharamia huduma na vipuri vya magari haya kwa bei nafuu. alimaliza kusema Xiong.





from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PQsTi3
via

Post a Comment

0 Comments