Ticker

10/recent/ticker-posts

MASHTAKA MAWILI KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI

Bunge la wawakilishi liliitisha kura kwa ajili ya mashitaka mawili. Shtaka la kwanza likiwa ni kutumia vibaya mamlaka aliyonayo lililotokana na madai ya kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alijaribu kuishinikiza Ukraine kutangaza uchunguzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa na muwania urais kupitia chama cha Democrats, Joe Biden. ,

Shtakala pili lilikua ni kuzuia shughuli za bunge la Kongresi kwa sababu rais anadaiwa kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi yake, kwa kukataa kutoa nyaraka za ushahidi na kuwazuia wasaidizi wake kutoa ushahidi katika uchunguzi huo.

Kura katika kipengele cha kwanza cha uchunguzi, cha kutumia vibaya mamlaka zilikuwa 230 ndiyo na 197 hapana na kipengele cha pili cha kuzuwia utendaji wa Kongresi zikawa 229 ndiyo na 198 hapana.

Kuchuguzwa kwa Trump kunamuweka katika nafasi za marais wengine wawili tu katika historia ya taifa hilo Andrew Johnson na Bill Clinton  na sasa Bunge la Seneti litaendesha kesi juu ya urais wake.

Hata hivyo chama cha Republican kina wawakilishi wengi katika Bunge la Seneti na hivyo anatarajiwa kushinda kesi hiyo na kusalia madarakani.

Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani, Nancy Pelosi amefafanua kuwa hatopeleka waraka uliopitishwa kumuondoa Rais Donald Trump madarakani hii leo kwenye Bunge la Seneti, mpaka  pale viongozi wa juu wa Seneti watakaporuhusu hatua hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2EwPrz5
via

Post a Comment

0 Comments