MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA BANDARI YA KASANGA,KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU YASHIKA KASI

  Masama Blog      
 Shughuli za ujenzi wa miundombinu ukiendelea katika Bandari ya Kasanga mkoani Rukwa.Bandari hiyo ni ya pili kwa ukubwa katika bandari zilizopo ndani ya Ziwa Tanganyika ambapo TPA imeamua kuboresha miundombinu yake.

 Sehemu ya upanuzi wa gati ya bandari ya Kasanga ukiendelea kwa kuwekwa mawe ya kokoto na nondo 

 Baadhi ya mafundi wakiwa wamebaba mawe kwa ajili ya kwenda kuweka eneo ambalo ujenzi wa gati ya bandari ya Kasanga unaendelea katika eneo hilo.
 Mafundi wakisuka nondo kwa ajili ya kutengeza nguzo ambazo zitatumika kubeba gati ya bandari ya Kasanga iliyopo Ziwa Tanganyika mkoani Rukwa.

 Moja ya meli ya Mizigo kutoka nchini Burunfi ikiwa katika bandari ya Kasanga ikipakia mifuko ya saruji inayotoka kiwanda cha Mbeya Cement 
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu unaondelea katika bandari ya Kasanga mkoano Rukwa.


*Kukamilika barabara ya lami Sumbawanga kwenda Kasanga yaongeza idadi ya malori yanayopeleka mizigo bandarini

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Rukwa

MENEJA wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama amesema bandari ya Kasanga ni ya pili kwa ukubwa kwenye ziwa hilo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  Tanzania(TPA) imeamua kufanya mradi mkubwa wa Sh.bilioni 4.764 ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanaotumia bandari hiyo kusafirisha mizigo kutoka nchini Tanzania kwenda nchi jirani.

Amesema kwa sasa katika bandari hiyo nyumba za wafanyakazi zinajengwa na kwamba tayari wameanza kuongeza gati ya sasa kutoka mita 20 mpaka mita 120 kwa  lengo ni kuruhusu meli zaidi ya moja kutia nanga kwa wakati mmoja kwa sababu meli kama Mv. Liemba ina ruti ndefu kwenye Ziwa Tanganyika ina urefu wa mita 71.4, hivyo maana yake katika gati hiyo gati ya sasa ya mita 20 tafsiri yake meli nyingine hawezi kukaa. 

Salama ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini waliopo katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA).

Ambapo mbali ya ujenzi wa miundombinu ya bandari hiyo, waandishi wameshuhudia barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Sumbawanga mjini hadi Bandari ya Kasanga ikiwa ni mkakati wa Serikali kuhakikisha bandari hiyo inafika kwa urahisi ikilinganishwa na awali kabla ya kutengenezwa.

Akizungumza zaidi kuhusu bandari hiyo Salama amesema baada ya kuona gati ya eneo hilo ni dogo, kiasi cha kusababisha meli zisirubiane na kusababisha kukaa muda mrefu bandarini. TPA imeliona haja ya kuongeza urefu wa gati hilo na sasa urefu utakuwa mita 120."Tafsiri yake sasa itakuwa na uwezo wa kuweka meli mbili mpaka tatu kwa wakati mmoja kulingana na urefu wa meli, kutakuwa hakuna tena kusubiriana.Huu ni uboreshaji mkubwa kupata kutokea. 

"Pia tunaweka sakafu ngumu pale eneo bandari kuhakikisha kontena zinaweza kukaa bila tatizo , kwani tunamatarajio na tumeanza kuzungumza na mfanyabiashara mmoja ameonesha nia ya kutaka kushusha kontena kwenye Bandari ya Kasanga, likifanikiwa na huu uwekezaji ambao unaofanyika maana yake kwamba azma ile ya uwekezaji na matokeo ya uwekezaji yatakuwa yamefikiwa,"amesema Salama.

. Ameongeza katika ujenzi huo wa miundombinu TPA inajenga nyumba za wafanyakazi wa bandari ambazo ziko mbili na hivyo wafanyakazi na familia zao watakaa katika nyumba hizo, hivyo hawatakuwa na shida kwenda mahali pengine na kwamba wanaishukuru  Serikali kwa kipekee kwa kuwezesha kuboresha barabara ambayo ilikuwa imebaki kama kilometa kama 50 hivi ambayo sasa imewekwa lami kutoka Sumbawanga mpaka Kasanga. 

"Kwa hiyo ile barabara ya kilometa 90 ambayo mwanzo ilikuwa changamoto kubwa ni amini sasa hivi tu nazungumzia barabara ile kukamilika kufikia mwishoni mwa Desemba au kama ikichelewa sana Januari itakuwa imekamilika yote kabisa.Inaleta matokeo makubwa sana, sasa Bandari  ya Kasanga ya sasa ukiiangalia mwaka jana ilikuwa inachangia karibu asilimia 19 ya mapato. 

"Unapozungumzia zile Shilingi bilioni 4.148 tulizopata mwaka jana kwenye mwaka wa fedha 2018/19 kama gawio kwa Serikali, Bandari ya Kasanga ilichangia asilimia 19 ya mapato lakini ukiiangalia kwenye mwaka huu wa fedha tulianza nao 2019/19 mpaka sasa miezi mitano hii kuanzia mwezi wa 7 mpaka 11 tayari bandari hii imeishatuingizia karibu Sh.milioni 490 , hivyo mchango wake umeongezeka kutoka asilimia 19 za mwaka jana kwenda mpaka asilimia 29,:amesema.

Salama amesema katika mapato Bandari ya Kasanga ya Sh.million 288 unaona karibu Sh.milioni 100 zimechangiwa na Kasanga, uwekezaji ule ambao Serikali inaufanya Kasanga kupitia TPA ni muhimu na una tija kwa Taifa kwani umeshaanza kuonesha kupandisha huduma na kuvutia wateja hasa wenye meli kutumia bandari ya Kasanga, hivyo ni uwekezaji sahihi. from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Mjnm2q
via
logoblog

Thanks for reading MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA BANDARI YA KASANGA,KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU YASHIKA KASI

Previous
« Prev Post