Ticker

10/recent/ticker-posts

Mama lishe ajishindia bodaboda kupitia promosheni ya ‘TUNZA, UTUNZWE na M-PAWA’

 Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Meneja wa Huduma ya M-PAWA kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche (kulia) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam akionesha kadi ya pikipiki wakati wa makabidhiano ya zawadi yake hiyo. Kushoto ni Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu akionesha funguo za pikipiki. Akishuhudia kulia ni Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 . Meneja wa Huduma ya M-PAWA kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (hayupo pichani) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanya uwanja wa Sahara, Mabibo. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 . Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (hayupo pichani) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanya uwanja wa Sahara, Mabibo. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania
Mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana mwenye miaka 26 (kushoto) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam akisindikizwa na wapambe kwenda kukabidhiwa zawadi yake. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.

Benki ya CBA na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom jana imemkabidhi mshindi mmoja wa promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ pikipiki mpya aina ya ‘Boxer BM125’ yenye thamani ya shilingi milioni tatu baada ya kuibuka kidedea katika droo ya wiki ya kwanza ya shindano hilo. 

Mshindi huyo, Bi. Leticia Yohana (26) mkazi wa Mabibo makutano jijini Dar es Salaam anayejishughulisha na kazi ya upishi ‘mama lishe’ alionekana mwenye furaha na bashasha alivyokabidhiwa pikipiki hiyo mpya katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya Sahara, Mabibo.

“Kwa kweli haikuwa rahisi kuamini kwamba nimeshinda. Ninafuraha sana kuwa mshindi wa pikipiki hii leo. Nimekuwa mtumiaji wa huduma ya M-Pawa kwa muda mrefu, kwa kuweka pamoja na kukopa kwa ajili ya biashara yangu ya chakula,” alisema Bi. Yohana.

“Nitatumia pikipiki hii kama fursa ya kuendelea kujikwamua kiuchumi kwa kuitumia kwa matumizi ya kubeba abiria, yaani bodaboda. Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashawishi Watanzania wenzagu watumie M-Pawa ili nao waweze kupata nafasi ya kushinda,” aliongeza mshindi huyo.

Akimpongeza mshindi huyo, Meneja wa Huduma ya Kibenki ya M-Pawa kutoka CBA, Bi. Gloria Njiu alisema benki ya CBA inajivunia kubadilisha maisha ya watanzania kwa kupitia promosheni hii ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ inayotoa zawadi kedekede ikiwemo zaidi ya pesa taslimu shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa wateja wao. 

“Promosheni hii ya wiki sita inawapa fursa Watanzania kushinda mara mbili ya akiba yao katika akaunti zao za M-Pawa, kushinda bodaboda kila wiki, na mshindi mmoja kuondoka na donge nono la fedha taslimu ya shilingi milioni 10,” alisema Bi. Njiu.

Akielezea zaidi kuhusu promosheni hii, Bi. Njiu alisema “Promosheni hii imelenga kuwazawadia watumiaji wazuri wa huduma ya M-Pawa zawadi mbali mbali. Mpaka sasa tumeshafanya droo mbili na kupata washindi 120 walioshinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 4, huku washindi 7 wakishinda pikipiki zenye thamani ya shilingi milioni 21 hadi sasa.”

“Mshindi mkubwa wa promosheni hii atazawadiwa shilingi milioni 10 kwenye droo ya mwisho hivyo tunaendelea kuwasisitiza watumiaji wa M-Pawa na wengine ambao hawajajiunga bado kujiunga na kuweka akiba na kurejesha mikopo mapema ili waweze kupata nafasi ya kushinda,” alieleza Bi. Njiu.

Kujiunga na M-Pawa, piga *150*00# kisha chagua M-Pawa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2roCKUc
via

Post a Comment

0 Comments