Ticker

10/recent/ticker-posts

Mafundi wa mizani waaswa kwenda na teknolojia ya kisasa

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mafundi mizani nchini wametakiwa kubadilika na kutumia tekonojia za kisasa ambazo zitachagiza ukuaji wa uchumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu  ya Biashara (CBE), wanaosoma mizani Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam alisema, teknolojia inabadilika hivyo ni wakati sasa wa kuendana na mabadiliko ili tusiachwe nyuma kibiashara.

Alisema wao kama watengenezaji na watoaji Mafunzo ya mizani wameamua kutumia mizani ya kisiasa ambayo itasaidia wafanyabiashara na wateja wao kupata bidhaa halisi kwa kiwango wanachohitaji.

"Wakati sasa umefika wa kutumia mizani sahihi yenye viwango vinavyohitajika ili kukidhi soko la Afrika Mashariki...naomba wanafunzi mnaosoma somo hili mkawe walimu kwa wengine kwakuwa mizani hii inatoa haki kwa anayeuza na anayenunua,"alisema Hazam.

Alisema wanafunzi wanaosoma somo hilo watachangia Maendeleo ya nchi kwani ni Idara muhimu kwa Maendeleo ya Taifa.Alisema mizani yao eanayotengeneza ni ya kisasa kwakuwa mtu anapata anachostahili na Ina alama maalumbya Serikali hivyo mtu akijaribu kuichezea ili amuibie mteja wake haufanyikazi.

"Tumeingia ubia na CBE kutoa elimu hii kwa wanafunzi wao tunaamini somo hili litaleta mabadiliko na kutoa haki kea wafanyabiashara na wateja endapo watatumia mizani ya kisasa,"alisema Hazam.Alisema wafanyabiashara wengi wamekuwa na tabia ya kuchezea mizani ya zamani kwa sababu ya teknolojia iliyotumika hivyo kusababisha wateja kukosa haki yao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa  Mafundi Mizani, Mpasi Hassan ambayr hi Mkurugenzi wa Kampuni ya Henecha Scale alisema,  mafunzo hayo ni muhimu kwao hasa nyakati hizi za mabadiliko ya kiteknolojia.

Alisema wanaamini watejengewa weledi utakaoleta mabadiliko na ukuaji wa uchumi.Naye, Naibu Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaalam, Respius Kasmir, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali, alisema Chuo kinatakiwa kitoe mafunzo yanayoendana na matakwa ya walengwa hivyo waliamua kuungana na Sahel kwakuwa Ni wadau muhimu wa mizani.

Alisema chuo hicho ndio pekee Afrika Mashariki kinachotoa kozi ya mizani ambapo nchi ya Kenya nayo huwa wanatoa kozi fupi.

"Ushirikiano na wadau unachangia kuleta bidhaa zenye ubora ambapo ndani ya miaka mitatu tumepata mabadilko ya ongezeko la juu la wanafunzi wa somo hilo ambapo kwa sasa ni  asilimia 40 Hadi 50,"alisema Casmir.
 Mhadhiri Msaidizi katika Chuo cha Biashara (CBE) Boniface Mtasingwa  akimkabidhi Cheti cha mafunzo ya Mizani Bartholomeo Kavishe katika hafla iliyofanyika Chuo cha Biashara CBE Jijini Dar es Salaam
 Rais wa Fani ya Mizani katika Chuo cha Biashara (CBE) Nicholaus Kiyuga akionesha mmoja ya mizani ya kisasa wakati  utoaji vyeti kwa mafundi mizani iliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja  kati ya watendaji wa kamapuni ya Sahel waigizaji na watengenezaji mizani pamoja watendaji wa chuo cha Biashara (CBE)
 Naibu Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaalam, Respius Kasmir, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali akizungumza wakati wa upokeaji wa mafunzo kwa mafundi mizani waliokuwa wakipata mafaunzo hayo katika chuo cha Biashara Kampasi ya Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam akizungumza kuhusiana na umuhimu wa mafunzo kwa mafundi mizani kutokana na teknolojia hiyo kubadilika kila siku wakati wa utoaji vyeti kwa mafundi mizani katika Chuo cha Biashara (CBE).
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2EZBudb
via

Post a Comment

0 Comments