KIFAA CHA KUDHIBITI WIZI WA PIKI PIKI NA VYOMBO VYA MOTO HIKI HAPA

  Masama Blog      
Na Grace Gurisha

MENEJA Mauzo na Masoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology, Mohamed Kaddy amesema wameleta  kifaa maalumu chenye uwezo wa kudhibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto.

Kaddy aliyasema hayo leo Desemba 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho, ambapo alisema kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana na mmiliki atapata taarifa kupitia simu yake ya mkononi.

Meneja huyo alisema teknolojia hiyo ni rahisi, "Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu, lakini pia kama kuna mtu amesimama katika pikipiki yako utajulishwa”,.

"Kifaa hichi maalumu kitafungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja atapata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika simu yake ya mkononi na pia hata akipoteza simu yake anaweza kutumia simu ya mtu mwingine na kupata taarifa kifaa chake kilipo," alisema 

Alisema mfumo huo husaidia kudhibiti udanganyifu wa madereva au marafiki katika matumizi ya umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki kupata taarifa kwa haraka pale chombo chake kikitaka kuibiwa au kushikwa na mtu, pia mfumo huo utamsaidia mtu kuzima au kuwasha chombo mahali popote atakapokuwa, kama umeibiwa unauwezo wa kuizima pikipiki yako kabla haijafika mbali," alisema

Alisema kifaa hicho tayari kimeshaanza kuuzwa kwa bei nafuu, hivyo madereva wajitokeze kwa wingi kununua ili kudhibiti wezi kutokana na wimbi la wizi wa Bodaboda linaloendelea hivi sasa.

Pia, alisema wanafunga vifaa kwenye nyumba kwa mfumo wa kisasa ambapo hata mwizi atakapokwenda kuiba hata gundua kama kuna kifaa cha usalama kimefungwa kwa hiyo itakuwa ni rahisi yeye kukamatwa kwa sababu kifaa kitaonesha kuna mtu ameingia.
 Meneja Mauzo na Msoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali yabkiteknolojia ya MD Technology, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kifaa cha kisasa cha kuzuia wizi wa vyombo vya moto.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya MD Technology, Brian Kessy akiwaeleza madereva wa Bodaboda faida ya kifaa hicho ambacho kitawasaidia katika suala nzima la ulinzi wa pikipiki zao
 Mtaalamu wa Mifumo kutoka MD Technology, Salum Mntitiwa akionesha jinsi ambavyo kifaa hicho kilivyofungwa na kuunganishwa na simu ya mkononi kinavyoweza kufanya kazi kwa kuliweka gari katika hali ya usalama,from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RUIQGO
via
logoblog

Thanks for reading KIFAA CHA KUDHIBITI WIZI WA PIKI PIKI NA VYOMBO VYA MOTO HIKI HAPA

Previous
« Prev Post