KAMPUNI YA WANANCHI GROUP LTD NCHINI TANZANIA YAMTANGAZA RASMI MENEJA MKAZI

  Masama Blog      
KAMPUNI ya Wananchi Group Ltd hapa nchini Tanzania  imetoa kauli kwa vyombo vya habari ya kumtangaza rasmi, Meneja Mkazi nchini Tanzania wa Wananchi Group kupitia Kampuni hiyo,Sanctus Mtsimbe.

Taarifa ya Kampuni hiyo kwa vyombo vya habari ambayo wametoa leo jijini Dar es Salaam kuwa kampuni yao amemteua  Kennedy Ojungo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simbaNet. 

Imeeleza kwamba Ikampuni hiyo inatoahuduma tofauti tofauti  katika nchi nyingi barani Afrika ambapo miongoni mwa nchi zilizokuwa zinafanya kazi na kampuni hiyo ni pamoja Kenya, Uganda, Tanzania, Malawi na Zambia. 

Aidha katika taarifa hiyo ilisema Mtsimbe amepitia katika uongozi mbalimbali ikiwemo Ofisa Mwandamizi wa SimbaNet Afrika  Mashariki, pia tayari aliwahi kuwa na nafasi ya Meneja Mkuu wa Teknolojia ya Mawasiliano ya Airsys (Uingereza) na Meneja Mauzo wa Mkoa kwa Mawasiliano ya Danimex ya nchini  Denmark. 

Pia Kennedy ana uzoefu mkubwa katika tasnia ya Mawasiliano baada ya kufanya kazi katika uwezo wa juu wa mashirika anuwai ya kimataifa.  Aidha Kikundi cha Wananchi hufanya biashara mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya makazi, mtandao na huduma za burudani na huduma za mawasiliano ya biashara .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/392k6Cz
via
logoblog

Thanks for reading KAMPUNI YA WANANCHI GROUP LTD NCHINI TANZANIA YAMTANGAZA RASMI MENEJA MKAZI

Previous
« Prev Post